Tuesday, August 4, 2020

Lissu ampa za uso Jaji Mutungi amtaka akoseme sheria ya nembo ya taifa

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amesema Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi akasome sheria ya nembo ya taifa ya mwaka 1971.

“Mwambieni Msajili wa Vyama vya siasa akasome sheria ya Nemboza taifa ya 1971 ili ajiridhishe kama wimbo wa taifa ni moja wapo ya nembo za taifa zinazolindwa kisheria kabla hajatoa vitisho vya bure kama hivi,” Lissu aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter.

Lissu aliongezea kuwa ” Ataje sheria iliyovunjwa kama ipo kabla ya hajatoa kauli za aina hii,”.

Leo Jaji Mutungi ameionya Chadema kwa kuvunja sheria kwa kuongeza ubeti wa tatu kwenye wimbo wa taifa jana wakati wakipitisha jina la atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/04/tundu-lissu-ampa-za-uso-jaji-mutungi-amtaka-akoseme-sheria-ya-nembo-ya-taifa/

No comments:

Post a Comment