Wednesday, August 5, 2020

Lissu Amng’ata Sikio Membe

ImageMakamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amemkaribisha rasmi kwenye upinzani aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje Bernard Membe na kumtaka ajikaze kwani kwenye vyama vya upinzani ni pagumu.

Lissu amesema hayo kwa Membe ambaye ni mtiania wa kugombea nafasi ya urais kupitia tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo wakati alipopewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano mkuu wa chama cha hicho  unaoendela leo Agosti 5, 2020 jijini Dar es salaam.

‘Kaka yangu Ben nakukaribisha kwenye mapambano lakini nikwambie tu huku ni kugumu” amesema Lissu.

Membe alitangaza uamuzi wa kujiungea kwenye chama cha mapinduzi (CCM), na kurejesha kadi ya uwanachama wa chama hicho kabla kutambulishwa rasmi kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo Julai 17,2020.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/05/lissu-amngata-sikio-membe/

No comments:

Post a Comment