Thursday, August 6, 2020

Dondoo za leo: Waziri kikaangoni tuhuma za rushwa, Ndugai apigiwa debe Uspika na Mfanyakazi wa ndani ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari leo Agosti 07, 2020.

Habari hizo ni Waziri kikaangoni tuhuma za rushwa je unajua ni nani huyo?,  Job Ndugai apigiwa debe Uspika bunge lijalo kulikoni? na Mfanyakazi wa ndani ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kulawiti mtoto wa mwaka mmoja je unajua ni wapi tukio hilo limetokea soma habari hizi kwa kina.

Karibu msomaji wetu;

WAZIRI KIKAANGONI TUHUMA ZA RUSHWA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mary Mwanjelwa, amehojiwa Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kutoa rushwa wakati wa kura za maoni.

Mbali na Mwanjelwa, wengine waliohojiwa ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya mstaafu, Maryprisca Mahundi ambaye aligombea ubunge wa Viti Maalum (CCM) mkoani humo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Jacob Mwakasole, aliliambia gazeti hili jana kuwa mbali na Mahundi, Mwanjelwa ambao walikuwa wakichuana katika kinyang’anyiro hicho, kamati hiyo pia iliwahoji Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya Mbarali, Zabibu Baharam na Katibu wa UWT Wilaya hiyo, Veronica Mwembezi.

Soma zaidi

NDUGAI APIGIWA DEBE USPIKA BUNGE LIJALO

RAIS John Magufuli amempigia debe Spika wa Bunge, Job Ndugai, akisema atashangaa kama Bunge lijalo hawatamchagua kushika wadhifa huo kutokana na mambo makubwa aliyofanya ikiwamo kutungwa kwa sheria bora ya madini.

Magufuli alisema hayo jana jijini hapa alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makao Makuu ya chama hicho, baada ya kuchukua fomu ya kuomba kugombea urais katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) kupitia CCM.

“Namshukuru sana Spika, nitashangaa sana bunge linalokuja wakaacha kukuchagua wewe. Watasema nakupigia kampeni, nina haki kwani uliunda Tume ya Madini kwenda kuchunguza na ripoti akaileta na tukabadilisha sheria,” alisema.

Soma zaidi

JELA MAISHA KWA KULAWITI MTOTO WA MWAKA MMOJA

MFANYAKAZI wa nyumbani, Magige Thomas (21), mkazi wa Mtaa wa Rebu, Tarime mjini mkoani Mara, amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 5.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime, Veronika Mugendi, aliyesikiliza kesi hiyo ya jinai namba 419 ya mwaka 2019.

Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Salum, alidai mahakamani kuwa, mtuhumiwa huyo mnamo Agosti 5 mwaka jana mchana, akiwa mfanyakazi wa nyumbani maeneo ya Bomani, wakati wazazi wa mtoto huyo wakiwa wamekwenda kazini, alimlawiti mtoto wa mwajiri wake na kumsababishia maumivu makali.

Soma zaidi



source http://www.bongoleo.com/2020/08/07/dondoo-za-leo-waziri-kikaangoni-tuhuma-za-rushwa-ndugai-apigiwa-debe-uspika-mfanyakazi-wa-ndani-ahukumiwa-kifungo-cha-maisha-jela-na/

No comments:

Post a Comment