Monday, August 31, 2020

Dondoo za leo; Membe na kinachoiua CCM,CCM yataka asiwataje, Manzese kula ubwabwa wa Rungwe jumamosi

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo na Membe ataja kinachoiua CCM, CCM yataka wasiwataje ana mwisho ni juu ya Rungwe kuzindua kampeni zake jumamosi hii.

KINACHOIUA CCM

BERNARD Membe, mgomeba urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ametaja kitachoiua Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Amesema, sumu kubwa iliyopandwa na chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, ni mpasuko ndani ya chama hicho.

Membe ametoa kauli hiyo jana Jumatatu tarehe 31 Agosti 2020 katika uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya ACT-Wazalendo, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Membe aliyekuwa waziti wa mambo ya nje kuanzia mwaka 2007 hadi 2015 enzi za utawal wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kiwkete amesema, ndani ya CCM kuna mpasuko baina ya kundi la wanachama wapya na wa zamani.

Soma zaidi>>>

CCM YATAKA ASIWATAJE

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimetuma salamu kwa vyama vya upinzani kwa kuwataka kuacha chokochoko na wasioutakia mema nchi yetu huku kikitoa rai kwa wapinzani kuacha kutaja taja majina ya viongozi wao.

Akizungumza leo jijini Dodoma ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphery Polepole amesema kabla ya kusoma majina ya wagombea waliopitishwa kugombea ujumbe w baraza la wawakilishi ni vema kwanza akazungumzia mwenendo wa kampeni unavyoendelea kule Zanzibar na siasa zake.

Hivyo amesema kwamba “tungependa kuujulisha umma ya kwamba Chama Cha Mapinduzi tuko vizuri mno kwa maana ya wana CCM kule , wananchi wa kawaida kule, ambao wanatuelewa vizuri mno , wameupokea vizuri zaidi uteuzi wa ndugu yetu Hussein Mwinyi ambaye mpaka sasa hivi tumesema usikimbie.

UBWABWA WA RUNGWE JUMAMOSI

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Chaumma, Hashimu Rungwe, ametangaza kuzindua kampeni zake za urais wa chama hicho Jumamosi tarehe 5 Septemba 2020 Manzese jijini Dar es Salaam.

“Chaumma itaongea na wananchi 5 Septemba 2020 katika Uwanja wa Manzese Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana. Wananchi waje wasikilize, tunachowaambia. Wakija pale watapata kila kitu na watauliza maswali na tutawajibu.Wako watu wenye hamu ya ubwabwa waje tutajua tunawapatiaje,” amesema Rungwe



source http://www.bongoleo.com/2020/09/01/dondoo-za-leo-membe-na-kinachoiua-ccmccm-yataka-asiwataje-manzese-kula-ubwabwa-wa-rungwe-jumamosi/

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 1, 2020

Habari mdau wetu, Karibu utazame kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti nchini Tanzania.

Kipengele hiki Muhimu katika kuhabarika na Opera News kinapatikana kila siku asubuhi na kwa ujumla yapo magazeti mbalimbali yaliyosheheni habari za kisiasa, burudani, michezo na elimu.

  



source http://www.bongoleo.com/2020/09/01/habari-kubwa-za-magazeti-ya-tanzania-leo-september-1-2020/

Sunday, August 30, 2020

Dondoo za leo; Siku 100 za Lissu Ikulu, Aaaga dunia kwa kulipukiwa bomu, UVCCM wamvaa

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na NA SIKU 100 ZA Lissu ikulu, alipukiwa na bomu na mwisho ni juu ya UVCCM kumvaa Maalaim Seif

SIKU 100 ZA LISSU

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Tundu Antipas Lissu katika muendelezo wa kampeni zake jijini Dar es salaam ambapo leo Agosti 30 zimefanyika katika viwanja vya Liwiti Tabata amesema Nchi inahitaji maridhiano ya kitaifa.

Amesema katika siku 100 za kwanza baada ya kupata ushindi katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28, ataunda tume kwa ajili ya upatanishi na ukweli ili kuvumbua mabaya yanayofanyika katika nchi.

ALIPUKIWA BOMU

Mtoto mwenye mwenye umri wa miaka 9 katika kijiji cha Kasumo kata ya Kajana wilayani Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu Agosti 28, 2020.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kigoma Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi James Manyama amesema,

”Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Abas Jeras  mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Lemba kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo tarehe 28 mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuokota Bomu bila kujua na kuanza kulichezea kisha bomu hilo kuripuka na kusababisha apoteze maisha”.

Soma zaidi>>>

UVCCM WAMVAA

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umelaani kauli zinazodaiwa kutolewa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kwa mujibu wa UVCCM, kauli hizo zinaashiria uvunjifu wa amani wakati huu wakati huu wa kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ; na zimekiuka  tamko la vyama vya siasa la kuendesha kampeni za kistaarabu.

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Mussa Haji Mussa aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa kauli zilizotolewa na mgombea huyo, zina lengo la kuwatia hofu wananchi wasijitokeze kupiga kura na hazikubaliki.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/31/dondoo-za-leo-siku-100-za-lissu-ikulu-aaaga-dunia-kwa-kulipukiwa-bomu-uvccm-wamvaa/

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 31, 2020

Habari mdau wetu, Karibu utazame kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti nchini Tanzania.

Kipengele hiki Muhimu katika kuhabarika na Opera News kinapatikana kila siku asubuhi na kwa ujumla yapo magazeti mbalimbali yaliyosheheni habari za kisiasa, burudani, michezo na elimu.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/31/habari-kubwa-za-magazeti-ya-tanzania-leo-august-31-2020/

Saturday, August 29, 2020

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 30, 2020

Habari mdau wetu, Ikiwa unmalizia wikiendi leo Jumapili ya August 30, 2020 Karibu utazame kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti nchini Tanzania.

Kipengele hiki Muhimu katika kuhabarika na Opera News kinapatikana kila siku asubuhi na kwa ujumla yapo magazeti mbalimbali yaliyosheheni habari za kisiasa, burudani, michezo na elimu.

 

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/30/habari-kubwa-za-magazeti-ya-tanzania-leo-august-30-2020/