Monday, January 27, 2020

USIKUBARI KUWA MLINZI WA PENDO LA MWINGINE UKIAMINISHWA WEWE NI ZAIDI YA ALOKUTANGULIA⛔️


Dunia 🌏 inabyokimbia kuliko kuwa na MPENZI ni bora kuhudhuria nyumba za KU-BET ukibahatisha USHINDI WA MPIRA ⚽️
Mahusiano na Ndoa za sasa zinajengwa kwa FARAJA 💯 baada ya walopendana kushindwa kufikia ahadi walojiwekea kabla ya kuianza safari husika.
Wengi wamebakia kwenye MAHUSIANO NA NDOA zenye migogoro ili kulinda WATOTO, MALI na wengine wanakwenda mbali zaidi kulinda HESHIMA MAENEO WANAYOISHI lakini ndani wanaugulia sana😭😭
Kwa sasa FARAJA ndilo suruhisho la WANA MAHUSIANO/NDOA ili kubakia na kivuli kwamba ana MWENZA huku wakiangukia kwenye MAPENZI YA MICHEPUKO japo ku-reduce stress 😂😂
Ndo maana USALITI imekuwa IBADA YA MAHUSIANO NA NDOA nyingi kwa sababu TULIO WENGI TUNAMILIKI WENZA WA WENGINE 💯
Kwa sasa kumpata Mwenza FRESH ni kama kutafuta MANABII WA UKWELI 😂😂
Wengi twajikuta tunazama kwenye MAPENZI YA MKOPO kwa mhusika kushindwa kusababisha FURAHA KWA MWENZA WAKE lakini ukirudi kwenye uhalisia MOYO HAUPENDI MARA MBILI ila mara moja tu 💯
Baada ya MOYO kuumizwa na aliyechaguliwa nao ni MAPAMBANO YA KUJIHAMI na akitokea mtu japo wa kuupa MOYO FARAJA kuna nafasi ya URAFIKI ambao utaambatana na MAZOEA pengine unaweza kupata UPENDELEO yaani utakuwa BADALA na sio MBADALA WA ALIYEPENDWA kwani tayari anaishi MOYONI 💯 pamoja na yote ufanyayo ili kuleta FARAJA maana hujapendwa ila unabakia kuwa MLINZI WA PENDO LA MWINGINE.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/usikubari-kuwa-mlinzi-wa-pendo-la.html

No comments:

Post a Comment