Thursday, January 30, 2020

Hivi unajua maana ya Ex wewe?

Related image

X ni matapishi, ndiyo hata wewe kama ushawahi kuwa X wa mtu basi ni tapishi la mtu (mtuaeche sisi ambao tulijitunza) sasa shida ni pale ambapo wewe upo na mpenzi wako lakini kila siku unatishwa na X wake. Yaani badala ya kutulia na kufurahia mapenzi na mtu wako kila siku wewe ni kuangalia ma X wa mwanaume/mwanamke wako na kujipimisha nao.

Mara hawa wamenizidi pesa, ooo sijui wamenizidi six pack, sijui ni ma handsome zaidi yangu. Ndugu yangu alishawaacha hata kama ni yeye aliachwa lakini inamaana kuwa hawaendani, kaa tulia huo wasiwasi utamfanya mwanamke wakoa kukimbie kwakua kila dakika ni kama unamkumbusha kuwa umekosea kuwa na mimi X wako anafaaa zaidi. Hata kama una ule uhansome wa ndani, una six pack za koromeo, jiamini kashakupenda wewe tulia!

Dada zangu sasa, yaani ndiyo mnachanganyikiwa kabisa, unamfollow mpaka X wa mwanaume wako, akipost picha, status unaona unajilinganisha, mbona ana tako zaidi yangu, sijui mfupi zaidi yangu, kanizidi hiki kanizidi kile, atakua alikua anamfanyia vile.

Anikuambie kitu alichokuzidi ni dhambi tu ila angekuzidi na vingine angeshaolewa na huyo mtu, huyo ni tapishi tu achana nalo, sasa kama unajilinganisha na mtu aliyeachwa unataka kuwa kama yeye inamaana na wewe unataka uachwe? Acha kujilinganisha, jipendi hivyo hivyo, hata kama una ule uzuri wa ndani kama kakutongoza basi jua ana kutaka wewe alaaa!

Najua mshaanza kusema mbona kuna watu wanarudiana na ma X wao, kwanza wakwako hajarudiana naye hivyo acha wasiwasi, ila kuna wengine ni Kuku wanakula matapishi hakuna namna, yaani ujilinganishe usijilinganishe wao hawaachi, hata ungekua mzuri kama mabinti wa kipare (mnabisha nini sasa) basi bado angechepuka tu ni Kuku tu hivyo kaa tulia!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/hivi-unajua-maana-ya-ex-wewe.html

No comments:

Post a Comment