Thursday, January 30, 2020

UMEKUTANA NA MWANAUME KWENYE MITANDAO NA HAMJAWAHI ONANA? FANYA HIVI.


Related image
 (1) Chat naye kama huna mtu, kama huna kazi ya kufanya! Usivunje mahusiano yako kwaajili ya mwanaume wa mitandao ambaye hujawahi kumuona, wengi wanakua ni waume za watu au matepali ambao hata picha walizoweka si zao. Najua unadanganywa na video call au anaweza kukupigia simu saa nane usiku, dada wake zao ndiyo hawa wanakuja kunilalamikia kuwa waume zao wanachat mpaka saa tisa usiku. 

(2) Usimtumie picha yako hata ya sikio, hata kama umevaa nija usimtumie. Nyie ambao mnatuma matiti makalio na sijui nini mnajichoresha tu. Unajau ni kwanini, kuna wengine ni watu wanawafahamu lakini wanawachora tu, yaani mwingine ni rafiki yako kachukua picha za Mnigeria kaweka anakuchora kumbe mko naye ofisini. Hawa ni wale ambao hawatakivideo call wanakuambia kuwa simu ina matatizo. Kama picha zako anataka achukue kama wengine kwenye mitandao. 

(3) Usije ukamtumia pesa hata kama akikuambia kuwa Mama yake anahitaji elfu tano la sivyo atakufa, ni uongo! Kama zinakuwasha na unataka kutumia tu mwanaume nitumie hata mimi nikalipie zile soda za watu kwa Mangi! 

(4) Acha kumuambia mambo yako, sijui unafanya kazi gani, sheemu gani, kipatro flani, sijui hiki na kile, unajenga unamuambia, umenunua gari unamuambia kama mume wako wakati hata hujawahi kumuona.

(5) Mahusiano ya kwenye mitandao yanaanza baada ya kukutana, tena si kukutanahotelini, kukutana, wewe kujua anafanya kazi na ufike. Haiishii hapo, wewe kujua ndugu zake na kuhakikisha kuwa ni ndugu au hata marafiki, hapo ndiyo unaweza kusema nina mpenzi tofauti na hapo mtu ambaye unachata naye hujawhai kuoanana naye, hujui anafanya wapi kazi na hujui anachat wapi ni kujidanganya kuwa ni mpenzi wako. Yaani ni kama mimi ninavyoamini kuwa yule Mtoto wa kwanza wa Beyonce ni wakwangu! (Unabisha nini sasa unanijua mpaka useme hatujafanana naye)

 (6) Acha kumtambulisha kwa ndugu zako, rafiki zako, kumpost kabla ya kuonana naye, kujua anapofanya kazi, kujua kila kitu kuhusu yeye. Yaani hata kama alikuja unapokaa wewe, hajakupeleka kwake, akaja bwana, akawa mpenzi wako usimpost, aisee utajichoresha, wengi wanakua ni waume za watu unamtambulisha na kumkpos watu wanajua una mtu unajizibia riziki tu! 

(7) Asijekwenu kujitambulisha, akatuma watu, akatoa mahari kabla hajakupeleka kwao kukutambulisha na wakakukubali. Wengi ni waume za zatu na wakiona kuwa wewe una kamuelekeo ka maisah zaidi ya wake zao basi wanakua tayari wa lolote ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwenu na hata kufunga ndoa na wewe kumba ana wake watano nyumbani.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/umekutana-na-mwanaume-kwenye-mitandao.html

No comments:

Post a Comment