Thursday, January 30, 2020

Unapotaka kurudiana na mtu usirudiane kwakua yeye kabailika,

 Image result for rwandan girls

Unapotaka kurudiana na mtu usirudiane kwakua yeye kabailika,huwezi kupima kubadilika kwa mtu hata siku moja, anaweza kubadilika kwa maneno, akabadilika kwa muda au akaigiza kubadilika. Mtu pekee unayepaswa kuangalia kama kabadilika au la ni wewe.

Badala ya kuwaza je atanipiga tena basi waza akinipiga tena nitafanya nini? Badala ya kuwaza je ataendelea kuchepuka basi waza je akichepuka nitafanya nini? Badala ya kuwaza kama atacha kukutukana waza je akinitukana nitafanya nini? Ni lazima uwe na majibu ya hayo maswali na kama huna hayo majibu basi ni kazi bure hata ukirudi.

Rudi kwakua umebadilika, umekua mtu mpya, hunyanyasiki na wala hupigiki tena, lakini kama unarudi huku ukiwaza je kabadilika au la basi acha usiudi, kama huna majibu sahihi ya hayo majibu basi usirudi kwani kubadilika kwa mtu ni kati ya mtu na Mungu wake, si ndugu, si Iddi Makengo wala mtu mwingine yoyote anaweza kukuthibitishia kama kabadilika au la?

Hatua ya kwanza ya wewe kubadilika ni kujipenda wewe, kutambua kuwa maisha yako yanathamani, kutambua kuwa furaha yako ni ya muhimu na haipawi kumtegemea mtu yoyote yule.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/unapotaka-kurudiana-na-mtu-usirudiane.html

No comments:

Post a Comment