πππ
Zamani bwana nilikuwa nasikia tu wanawake baadhi hawapendi ndugu wa waume zao ila sasa mpaka wanaume baadhi yao hawapendi ndugu wa wake zao wakija jamaa anakuwa na kisirani utafikiri amelala na kuamka na nyoka aina ya kobra.

Sawa kuwa na kisirani lakini usitarajie na wakwako wakija watafurahiwa ikiwa ndugu wa mke wakija unawanunia ,pesa ya matumizi huachi makusudi kwani wamekuja kukaa moja kwa moja mpaka uvimbishe mashavu kama mpuliza tarumbeta wa shughuli ya kumtoa mwali???
Wewe historia yako tu ulivyokuja mjini kutafuta maisha ulifikia kwa ndugu ,kwa marafiki n.k mpaka ukalijua jijii na mitaa yake.
Labda nikwambie mtu akija kwako ukiona hana dalili ya kuondoka na anasema kijijini harudi mwambie nakutafutia kazi maana hapa mjini bila kazi ni mtihani sana na siyo kumwacha akae tu.
kubadili chanel za Tv ndani kama mwali laah hasha iwe mdogo wako ama shemeji yako maana kuna watu hawajui kujiongeza mpaka aongezwe kwahiyo waongoze kama wewe Ulivyosaidiwa na ndugu jamaa na marafiki mpaka ukayapatia maisha n sio kuwa na roho mbaya utadhani muuza sumu...

Kwahiyo tusiwachukie wageni ambao ni baraka kwa upande mwingine.
Watu hawafanikiwi kwasababu hawawakirimu wageni,ndio kwanza anawanunia halafu unapiga kelele mimi sifanikiwi, utafanikiwa vipi sasa wakati ukarimu huna zaidi ya gubu na roho mbaya.
Na wewe ndugu unae enda kukaa kwa ndugu usikae tu ndani kama mwali ukaridhika eti kwa dada yako kumbuka dada yako kaolewa wakikorofishana humo ndani mnatimuliwa wote nenda kasalimie ukiona hurudi kijijini shida waambie naomba mnitafutie Kazi na wewe Uwe na kwako.
Na nyie mashemeji mkienda msikae tu kisa kwa kaka yenu, mpaka nguo wataka sasa shemeji yako ndio akufulie utachokwa haraka na kupigwa teke kama mpira wa kona.....
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/mwanaume-kuwa-na-tabia-hizi-ni-ujinga.html
No comments:
Post a Comment