Huyo anafanya mzaha watu hata boyfriend hatuwapati alafu yeye anachezea ndoa alafu Mumewe akipata wa nje ataanza tafuta mganga si ndio uchawi wenyewe huo natamani huyo Mume wake apate Mke sahihi amkomeshe huyo Mwanamke sema tu Neno la MUNGU π Lina MSINGI yake lazima ifuate endapo kila mmoja wetu anataka kuingia mbinguni
✍️Kuna familia moja ya Baba, Mkewe na Watoto wao wawili, Mtoto mmoja anafanya kazi hospitalini na huyu mwengine ndio yupo form three
✍️Huyu Baba yeye katika maisha yake alishasema kwamba kipindi atakapooa atataka na kumuomba MUNGU ampe Watoto wawili tu kama wote ni Wakike sawa, kama wote ni wa Kiume sawa ama hatakama ni mchanganyiko pia sawa
✍️Basi bwana kweli MUNGU akawapa Watoto wawili huyu wa kwanza wa kiume na wapili wakike
✍️Kama tunavyojua maisha ya ndoa kuna kupanda na kushuka, mapenzi kuisha na kurudi vurugu za hapa na pale lakini mwisho inaposhindikana basi Wanandoa hutengana ama kuachana kabisa
✍️Basi ndoa hii pia ilikuwa na vihoja sana yani Mwanamke haishi vituko kwa Mumewe, japo Mumewe alivumilia sana lakini naamini ndani ya moyo wake alishasema kwamba siku itakuwa basi
✍️Akavumilia mpaka huyu mtoto wake alipofika la saba huyu Baba na nahisi katika Wanaume wote ni mara yangu ya kwanza kusikia akaamua kwenda hospital na kuweka njia ya uzazi wa mpango akaamua kufunga kizazi
✍️Alifanya hivyo baada ya kuona ameshamaliza kupata watoto aliowahitaji ni kumuomba tu MUNGU awape maisha marefu na afya njema basi akaenda kufunga kizazi bila kumtaarifu Mkewe
✍️Basi bwana maisha yakaendelea Mume akivumilia vituko vya Mkewe, uhuni ndio ulikuwa umekomaa sana kwa Mkewe na mengine madogomadogo kama anavyosema Mumewe
✍️Ikafika kipindi Mkewe akaingia kwenye mahusiano na kijana mmoja mdogo sana kwa Mumewe, yule Mama alichanganyikiwa sana na yule kijana kwani aliweza kumridhisha sana kitandani na kumpa mapenzi tele
✍️Kijana huyu alikuwa anajiweza anafanya kazi zake nzuri tu na japo yule Mama alikuwa na hela zaidi yake mtoto wa watu alijitutumua na kumuhudumia Mama japo kwa kidogo alichokuwa nacho
✍️Mapenzi kati yao yakawa motomoto Mama anachelewa kurudi nyumbani anarudi usiku sana wakati Baba na Watoto wameshalala, Baba hapewi tena haki yake ya Ndoa kama zamani na akipewa basi kwa mwezi ni mara mbili tu nyengine zote anapewa kijana
✍️Basi bwana huku na kule Mama akaanza kujisikia vibaya mara kizunguzungu, mara anahamu ya chakula fulani mara asubuhi anatapika akajua anamalaria kwenda hospital akapima malaria na mkojo akakutwa na mimba
✍️Sasa akaanza kuchanganyikiwa hii mimba ya nani ya Mume wangu ama ya hawara..
✍️Basi siku hiyo mwenyewe karudi nyumbani kamuandalia Mumewe chakula kizuri mapenzi motomoto mpaka Mumewe na watoto wakaanza kushangaa walipomaliza kula wakaenda chumbani kwa mahaba Mama akaanza kumtomasa Baba na kumwambia kwamba anamimba, wanategemea kuzaa mtoto wa tatu
✍️Baba ndio kushtuka unamimba❓ hapana hiyo mimba sio yangu sasa yale yote Mume aliyokuwa ameyaweka moyoni ndio yakamtoka gombana na Mkewe, Mama analia hii mimba yako , Mume anakataa , ndio Mume kuamua kumuonyesha Mkewe sasa ile alama ya operation aliyoamua kufanya kufunga uzazi
✍️Mama tena kumshuka lakini bado akawa mbishi hapana haiwezekani labda ulifanyiwa operation kwa magonjwa mengine kwanini ukaenda kufunga kizazi bila mimi inamaana gani unafanya jambo kama hilo kubwa bila Mkeo .
✍️Yule Baba akamwambia kama huamini kesho twende nikupeleke ukashuhudiwe na daktari basi kweli wakaenda mpaka hospital fulani maarufu nchini Tanzania πΉπΏ akachukuliwa file lake daktari ndio kumuhakikishia yule Mama kweli Mumewe alifanya hivyo .
✍️Basi ndio Mume kumuhoji yule Mama hiyo mimba ya nani yani uhuni wote unaoufanya unashindwa kutumia kinga mpaka unaleta mtoto asiye wa ndoa kwenye familia kwakweli sintoweza kukusamehe bora tuachane
✍️Yule Mama kwa aibu akamuomba sana Mumewe msamaha lakini Mumewe alimsisitizia hawezi kulea mtoto aliyekuwa sio wake kwahiyo aondoke
✍️Basi yule Mama akaondoka, akamuacha Mumewe na watoto wale wake wawili kwakuwa watoto wote walisema wanataka kubaki na Baba yao.
Ndoa na IHESHIMIWE NA WATU WOTE π MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA adhabu ( Waebrania 13:4)
✍️Katika maisha ya ndoa kama sio kusikia basi tumeona ama wenyewe inatutokea kwamba Wanawake ndio wenye kubeba familia, kila kinachotokea kwenye Ndoa kiwe kibaya ama kizuri Mwanamke ndiye anayetakiwa kukabiliana nalo bila kupinga .
✍️Ifike sehemu kwenye Ndoa zetu Wanawake tuishi kwa amani, upendo wa kweli na kutaka kweli kuwa kwenye hiyo Ndoa sio tu kwasababu ya uvumilivu uliofundishwa kwenye kitchen party basi ukavumilie hata yasiyovumilika .
✍️Ama uoga wa kuonekana umeachika na marafiki zako au ndugu au kuwazia ile harusi ya ghali sana mliofanya na hekaheka zote za kitchen party na sendoff zikakufunga wewe kwenye ndoa isiyoweza kurekebishika
✍️ Leo nimeumia sana kuamka asubuhi na kupata taarifa kwamba Mke wa shemeji yangu alikunywa vidonge ajiuwe kisa wamegombana na Mumewe
✍️ Magombano kwenye ndoa ni mengi Wanaume wanatupiga, wanatutukania Wazazi, wanalala nje kisa kagombana na Mkewe, yote hayo ya kuumiza moyo tunakutana nayo kwenye Ndoa lakini je wewe kama Mke unapokeaje matatizo yako ya Ndoa⁉️
✍️Ukinywa vidonge ama sumu ufe je utakuwa umetatua lile tatizo❓ Watoto wako unamuachia nani Mwanaume yeye hatajali umekufa wewe ndani ya miezi mitatu kaleta Mwanamke mwengine ndani , tena umkute huyu Mwanamke ni zao wa Nyoka ndugu yake shetani watoto wako watateswa sana .
✍️Maisha ni zaidi ya kuwa na Mume kwamba useme mimi baada ya kuolewa sasa maisha yangu ndio yamesimama kila anachotaka Mume wangu nifanye, HAPANA
✍️Ndoa ni mpango wa MUNGU wala hakuweka Ndoa kuwa adhabu bali alitaka tupendane kwa dhati, tuheshimiane,kila mtu amjali mwenziye, tuzae Watoto tuwalee vyema kwenye maadili mema na ya kumpendeza MUNGU na basi utakapoamua kuoa fulani ama kuolewa na fulani ni kifo tu kiwatenganishe sio umalaya, sio ulevi,sio hasira,sio kupigwa bali KIFO tu
✍️Lakini unapoona kabisa Ndoa yangu hii tumejaribu sana kuilea, tumekalishwa sana vikao na wakubwa na wasimamizi wa Ndoa lakini bado hakuna mabadiliko labda ni muda wa wewe kukaa pembeni na kuanza maisha yako upya kama unawatoto lea wanao anza upya
✍️SIO kwamba ukichana na Mumeo hutakula, hutavaa au wanao wanatishindwa kwenda shule na kuwa na maisha mazuri hapana..
✍️Muda ukifika kubali kuolewa unapoingia kwenye ndoa nenda na moyo wa ukomavu na ujasiri, tumikia vyema ndoa yako, lea vyema watoto wako na Mumeo, jiendeleze kifedha na kimasomo, usikubali kukaa na kuwaza ama kujutia kwanini uliingia kwenye Ndoa inayokupa mateso
✍️Bali changamoto zako za ndoa zikujenge kuwa Mwanamke hodari, Mwanamke imara, Mama wa mfano kesho Watoto wako na watu wengine wakuheshimu kwakuwa Mwanamke shujaaa
#ZINGATIAπ
Ndoa na IHESHIMIWE NA WATU WOTE π NA MALAZI YAWE SAFI π MAANA waasherati na wazinzi MUNGU ATAWAHUKUMIA adhabu (Waebrania 13:4)
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/heka-heka-za-ndoa-na-kungwi.html
No comments:
Post a Comment