Ladies
Mwanaume kabla hajaku-approach lazima akueshimu, lazima akupe thamani yako kama mwanamke ..na yeye kufanya hivi inatokana na namna ulivyojiweka kimuonekano na kitabia.. Fanya juu chini kwa akili yako kujua je mwanaume huyu anaenitaka ananieshimu, anaijua thamani yangu kama mwanamke au ni moja ya wale ambao mwanamke kwao ni sehemu ya kutolea stress zao za mwili baada ya hapo hauna tena thamani ya uanamke mbele yake
Fahamu kuwa mwanaume ni mtu bora sana katika kusoma tabia za mwanamke ...hivyo namna anavyokuapproach inatokana na namna ulivyojionyesha kwake kitabia na kimuonekano.
Namna unavyojiweka kimuonekano na kitabia ndivyo wanaume wa tabia Fulani watavyotaka kuwa na wewe, au kutokuwa na wewe, au kuogopa hata kukuapproach au kujichunguza kwanza tabia zao na mienendo ya maisha yao kabla hawajataka kuja kuzungumza na wewe kuhusu maswala ya mahusiano.
Ukijiweka kihuni wanaume watakao kuwa wanakuaproach wengi wao watakuwa wenye tabia za kihuni, na siku wanakuacha wanakuacha kihuni pia...ukijiweka kiheshima na kujipa thamani ya uanamke na kufahamu nafasi yako ni ipi asilimia kubwa ya wanaume watakao kuwa wanakuja kukuhitaji ni wenye kariba ya tabia unazoonyesha..
Dayari Yangu
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/ladies-fahamu-kuwa-mwanaume-ni-mtu-bora.html
No comments:
Post a Comment