Thursday, January 30, 2020

UKWELI KWANINI WANAWAKE NI VIUMBE MUHIMU HAPA DUNIANI.


Wanawake ni viumbe wa kipekee sana ulimwenguni, ngoja tuangalie haya machache wanayokumbana nayo.
1. Ni viumbe pekee wanaobadilisha jina lao la pili la asili kwa ajili ya mapenzi.
2. Ni viumbe rahisi sana kuwashawishi na wana uwezo mkubwa wa kushawishi. Ulimwengu na jumuiya za kimataifa zinatambua mchango wa wanawake.
3. Ni viumbe ambao hupenda kweli kutoka moyoni kabisa.
4. Ni viumbe ambao wanaweza kwenda kulala bila kula kuhakikisha tu watoto wake wamekula na wameshiba.
5. Ni viumbe ambao wanalia na kutoa machozi kirahisi kuonesha wazi jinsi walivyoumia ndani ya mioyo yao.
6. Usiku mzima anaweza akawa macho kama mwanae ni mgonjwa ili kuhakikisha yuko salama, wakati huo unaweza kukuta mume ndio kwanza anaota ndoto ya sita yuko fofofoo.
7. Wanaweza wakauza hata nguo zao kuhakikisha wanawalisha watoto wao na kuwaona wakiwa na furaha.
8. Wako tayari kutoa sadaka maisha yao kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto wao.
9. Hukaa jikoni wakivuta moshi bila kulalamika ili kuandaa chakula cha wanae na mume wake.
10. Ni viumbe ambao huamini mtu kwa asilimia 100% hakufahamu, humfahamu lakini aweza ongozana na wewe kwako kwenda kuanzisha maisha.
11. Hata kama wanakumbana na maumivu na uchovu wa kubeba mimba lakini bado huwa busy kuhudumia mumewe pamoja na watoto.
Tupate wapi viumbe kama hawa? Wanawake ni pambo la ulimwengu, wanawake ni maua, kuwa na mwanamke ndani ya nyumba kuna ukamilifu fulani mwanaume anaupata.
Wanawake jitunzeni, jiheshimuni, jueni majukumu na mipaka yenu, ninyi ni wa thamani mno, mliumbwa kuwa wasaidizi wa wanaume na sio supervisor wa mwanaume.
Apataye mke, amepata kitu chema.
Ila hii kitu yenu ya kupenda pesa kuliko mapenzi inawaharibia kweli CV zenu.
All in all Kwenu wanawake, Unajivunia kuwa mwanamke? Basi comment hapo chini kwa kijivuna kumshukuru Mungu kwa kuumbwa mwanamke, na share kadiri uwezavyo!
I CARE.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/ukweli-kwanini-wanawake-ni-viumbe.html

No comments:

Post a Comment