1. Kuwa na matarajio makubwa sana aingiapo katika mahusiano, kuwa na matarajio makubwa kuhusu ndoa. Na mara aingiapo katika ndoa hukuta mambo sivyo kama alivyotegemea.
2. Kuvaa nguo fupi zinazoonesha maungo yao, mwanaume anaejielewa hawezi kuoa mwanamke wa namna hiyo. Kwake ataona utafaa zaidi kama ukiwa mchepuko.
3. Kupenda pesa kupitiliza! ni kweli mwanaume anawajibika kumhudumia mwanamke, lakini ikifika kipindi wewe unawaza hela tu, mwanaume akikuambia hana hela umenuna. Kamwe hawezi kufikiri kukuoa. Utachezewa ili kuhakikisha pesa zake zimeenda halali na kuachwa.
4. Kuwa na masharti magumu kuhusu mwanaume unayetaka akuoe. Baadhi ya wanawake wana masharti magumu utafikiri fomu za mikopo ya benki ambayo inakaribia kufilisika. Mimi nakuhakikishia utagonga miaka 35 bado bila bila.
Unakuwa na vigezo vingi utafikiri wewe ni mkamilifu asilimia 100.
Unakuwa na vigezo vingi utafikiri wewe ni mkamilifu asilimia 100.
5. Kulengesha mimba huku ukidhani itakuwa njia nyeupe ya wewe kuolewa. Hili ni kosa kubwa sana ambalo limeibuka hivi karibuni.
Wengi hudhani kuwa ukibeba mimba yake lazima atakuoa. Sawa anaweza kukuoa ila machungu yake utakayoyapata baada ya kuingia ktk Ndoa utaomba half time mwenyewe.
6. Kupenda kujionyesha na kujikweza uonekane jinsi ulivyo wa gharama, sawa inawezekana ni wa gharama kweli ila hata wanaume wa gharama wapo vile vile.
Utaishia kuchezewa na kuachwa pamoja na kucheza kwaito kwenye Ndoa za wenzako. Na itakubidi ukumbuke muda haukusubiri wewe. Mwanamke ajikwezae hana busara kabisa.
Utaishia kuchezewa na kuachwa pamoja na kucheza kwaito kwenye Ndoa za wenzako. Na itakubidi ukumbuke muda haukusubiri wewe. Mwanamke ajikwezae hana busara kabisa.
7. Kutembea na waume za watu na vibabu vilivyostafu vinavyokula pensheni. Hiyo ni laana. Unajifungia baraka za kupata mume bora.
Au utaweza kupata mume ila malipo ya uliyokuwa ukiyafanya lazima uyapate hapa hapa Duniani. Kumbuka sheria ya "karma" :
Au utaweza kupata mume ila malipo ya uliyokuwa ukiyafanya lazima uyapate hapa hapa Duniani. Kumbuka sheria ya "karma" :
8. Utoaji wa mimba! Hili najua linafanywa na wengi sana na limekua janga kubwa sana. Laana ya umwagaji damu au kuua ni kubwa mno (rejea kitabu cha mwanzo habari ya Kaini na Habiri). Starehe ulipata na ukafurahi kabisa kuwa amekufikisha sasa iweje mimba uje uitoe? Kama umefanya hivyo nenda katubu kwa muumba wako na kama hujawahi basi kamwe usithubutu. Kila mtoto huja na baraka zake.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/mambo-ambayo-baadhi-ya-wanawake-hukosea.html
No comments:
Post a Comment