Friday, January 31, 2020

HIVI HUYU NI NDUGU KWELI AU NIMEINGIZWA MKENGE MIMI KHAAAAA!!!


Kuna mgeni tumekua nae kwetu kwa wiki sasa, wife alinieleza kuwa ni binadam yake mtoto wa shangazi yake, kiumri wana rika moja na wife.
Ukoo wa wife nawafahamu wote kule kijijini sasa madai ya wife kuwa ni mtoto wa shangazi yake yakawa yamenishtua ambapo Nikamuomba aniambie kinagaubaga ni shangazi yupi exactly anadai '' shangazi mwenyewe wewe humjui''.
Nikashangaa maana watu wengi kwao nawajua hata ambao sijawahi kuwaona taarifa zao ninazo na watoto wao.
Pia katika kukaaa kwake nyumbani kwangu hawajahi kuniita shemeji, bali huniita "mkuu" na ni kijana alionekana kuwa na hofu wakati wote ninapokuwepo nyumbani.
Alipoona nimembana sana kuhusu huyo mgeni kaanza kusema eti kama Sitaki ndugu zake wafikie kwetu niseme wazi, nikampigia ndugu mmoja alieko kule kijijini ugweno na kumuelezea kuhusu mgeni huyu na majina yake ambapo alidai ukoo wao una watu wengi labda mashangazi zao waliopo wilaya zingine Ingawa hata hivyo wengi anawajua ila Bahati mbaya huyo hajapata kumfahamu.
Nikapigia karibu watu wanne majibu yao yanafanana.
Nadhani wale watu nilioongea nao walimpigia simu wife kuhusu mm kuwaulizia yule jamaa, surprisingly Jana jioni narudi home naambiwa eti kasafiri asubuhi shughuli zake zimefikia mwisho eti kaomba wife amuagie kwangu.
Kwa kweli haijaniingia akilini!
Wadau mnaonaje ni escalate hili suala kwenye ngazi za juu kiukoo kupata majibu ya kuniridhisha? Ili kuchukua hatua stahiki?
PLZ NISAIDIENI MAANA NIMEJAA POVU HAKUKALIKI YAAN HUM NDANI..........


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/hivi-huyu-ni-ndugu-kweli-au-nimeingizwa.html

No comments:

Post a Comment