Ni matumaini yangu kwamba msomaji wangu uko poa. Karibu tena kwenye busati letu la mahaba, tujuzane mambo mbalimbali yahusuyo sanaa ya mapenzi. Tunaendelea kuidadavua mada yetu kama inavyojieleza hapo juu.
Leo tunamalizia kuangalia namna ya kumsaidia mwanamke mwenye tatizo hili kisha tutahamia kwa upande wa wanaume.
3. MRIDHISHE MUWAPO FARAGHA
Sababu nyingine inayosababisha mwanamke kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mwenzi wake, kama tulivyoangalia awali, ni mwanaume kushindwa kumridhisha wanapokuwa faragha.
Narudia tena kusema kwamba mapenzi ni kama sanaa nyingine yoyote ambayo ni lazima ujifunze ili uwe hodari. Huwezi kujua kupiga gitaa na likatoa muziki mzuri kama hukujifunza, vivyo hivyo kwenye mapenzi.
Wanaume wengi wana tatizo la kushindwa ‘kuwafikisha’ wenzi wao wawapo faragha na kwa bahati mbaya zaidi, wengi hawapo tayari kujifunza. Wanaishi kwa mazoea, wanashiriki tendo kwa namna ileile, hakuna ubunifu, hakuna kujifunza na matokeo yake, wanasababisha wenzi wao wakose msisimko wa kuendelea kushiriki nao.
Ndiyo! Atafurahia vipi kuwa na wewe faragha wakati anajua kwamba utamuacha njiani baada ya kumaliza haja zako na hutashughulika kwa chochote kuhakikisha na yeye anafurahi?
Ni muhimu kwa wanaume kujifunza namna ya kuwafurahisha wenzi wao wawapo faragha ili kudumisha uhusiano imara. Ni matumaini yangu kwamba mpaka hapo, wanaume watakuwa wamepata kitu cha kujifunza. Vipo vitabu vichache vya ufundi wa mapenzi vitakavyokusaidia kama una tatizo la kushindwa kumfurahisha mwenzi wako muwapo faragha. Wasiliana nami kwa namba za hapo juu.
KUKOSA HAMU YA TENDO KWA WANAUME
Baada ya kumaliza kuangalia tatizo la kukosa hamu ya tendo kwa wanawake, tuhamie sasa upande wa wanaume. Huenda ukashangaa kwamba hivi wanaume nao wanaweza kukosa hamu ya tendo? Jibu ni ndiyo na wanaoathirika zaidi ni wanaume ambao wapo ndani ya ndoa.
Hata hivyo, kushughulikia tatizo hili kwa upande wa wanaume ni rahisi zaidi kuliko kwa upande wa wanawake kwa sababu kimaumbile, hisia za wanaume zipo karibu sana tofauti na wanawake. Hata hivyo, ningependa msomaji wangu usichanganye kati ya kukosa hamu na upungufu wa nguvu za kiume.
Mada ya upungufu wa nguvu za kiume tutaijadili siku nyingine lakini leo ningependa tujikite zaidi kwenye kukosa hamu na kupoteza kabisa msisimko.
NINI HUSABABISHA HALI HII?
Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo la kukosa hamu ya tendo kwa wanaume lakini kama ilivyo kwa wanawake, chanzo kikubwa ni msongo wa mawazo. Sababu nyingine ni matumizi ya dawa kali, mfano wagonjwa wa kisukari au saratani hutumia dawa zinazopoteza kabisa msisimko wa mapenzi.
Sababu nyingine ni uchafu wa wanawake husika, kutoridhishwa na tabia za mke au mwenza wako na matatizo ya kisaikolojia ambayo huwa yanasababishwa na jinsi mwanamke anavyopokea udhaifu unaojitokeza awapo na mwenzi wake faragha.
MFANO HALISI
Jackob ni mwanaume anayeishi ndani ya ndoa. Wiki kadhaa nimewahi kukutana naye na alinitafuta kutokana na tatizo lililokuwa linamsumbua. Si vibaya nikawashirikisha wote ili tujifunze kitu.
“Mke wangu analea mtoto mdogo ambaye ana umri wa mwaka mmoja sasa. Tatizo la mke wangu, amekuwa akijisahau sana kisingizio kikubwa kikiwa ni mtoto. Zamani mke wangu alikuwa msafi, anaoga hata mara tatu kwa siku lakini siku hizi hali ni tofauti.
“Si ajabu ukamkuta hajaoga kutwa nzima, mwili mzima ananuka maziwa na mikojo ya mtoto. Hali hii inanifanya nipoteze kabisa hamu ya kuwa naye faragha, nafikiria kuchepuka, naomba ushauri, nifanyeje?”Ungekuwa wewe ndiyo mshauri, ungempa ushauri gani Jackob? Ungepata nafasi ya kumshauri mkewe, ungemwambia nini?
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/ufanyeje-mwenzi-wako-anapokosa-hamu-ya.html
No comments:
Post a Comment