Wednesday, January 29, 2020

😭FUTA MACHOZI


Kuwa mtu mzuri katika dunia hii yenye wingi wa lawama na visasi ni sawa na kuwa mlinzi wa GOLI uwanjani..
Haijalishi idadi ya magoli utakayo zuia langoni pako ila mashabiki wako watakuchukia kwa kushndwa kuzuia Goli moja lililo wapa ushindi wapinzani wenu..
🌾Udongo pamoja na uchafu wake lakin ndio huotesha mbegu nzuri za matunda yote matamu kama Apple...stroberry...zabibu..nanas..tikitii...
πŸ˜”Kumbe kamwe usiogope mabaya yatakayosemwa juu yako maana ndani yake kuna mengi mazuri ila wanajifanya hawaoni.
πŸ––πŸΌWengi hawapendi kushika mkaa wakihofia kuchafuka ila wanapenda sana chakula kilicho ivishwa katika mkaa.. Kuna watu hawakupendi lakini mafanikio yako yana wanyima usingizi na wanatamani wawe kama wewe.
πŸŒ‘Rangi nyeusi huchukiwa na baadhi kwa madai kwamba ni rangi ya msibani..lakini wapo ambao wanaipenda rangi hiyo kupita kiasi.
Kumbe Sio wote ambao wanakuombea mabaya..wapo wengi wenye kukutakia mema..
Futa machozi na utabasamu....
Upo gizani washa mshumaa ndani ya moyo wako utakao mulika kuta zote zenye simanzi...
Upweke
Kukata tamaa.na woga.
πŸ‘€Usiwaogope walimwengu maana furaha yao pale unapo shindwa.wafanye wavimbe kwa wivu na hasira wanapo ona ukifanikiwa....


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/futa-machozi.html

No comments:

Post a Comment