Friday, January 31, 2020

Japo mapenzi sio rahisi,kama unampenda kweli mruhusu akumiliki!


Image result for lethal lipps

Watu wengi huwa tuna tabia ya kushirikisha watu kwenye maamuzi yahusuyo mioyo yetu.Jambo hili si sahihi,kwanini?? Si sahihi kwa sababu unachokiwaza na kuhisi(feel) juu ya mtu anaetaka awe nawe kimapenzi havina uhusiano wa Moja kwa Moja na mawazo ya mtu mwingine.Kila mtu ana hulka yake,huwezi mfahamu mtu kiundani kwa kupitia mawazo ya watu wengine ambao ukute nao hawana upeo mkubwa was kumsoma mtu na kujua tabia zake.

Unaweza mkataa mtu kwa kuambiwa na rafiki yake kwamba jamaa/binti hajatulia.Miezi kadhaa baadae mtu huyo akahitaji kuwa na wewe,je Nani hajatulia kati ya hao wawili??

Hakuna ardhi bila mawe,ili uipate ardhi yenye rutuba lazima uihangaikie.Mfanye umpendaye awe vile unavotaka muweze elewana muishi pamoja maana tabia si Kama kabila useme haibadiliki.Ilhali ikishindikana Basi jiengue.
Jenga tabia ya kumsoma mtu wewe binafsi,na si kupitia marafiki zake.Sikiliza hitaji la Moyo wako na ulitekeleze.

Endesha mapenzi yako vile utakavyo na mtu umpendaye.Pia usisite kukomaa pindi ukataliwapo,maana vyenye uthamani ni vigumu kuvipata!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/japo-mapenzi-sio-rahisikama-unampenda.html

No comments:

Post a Comment