Monday, January 27, 2020

AINA ZA WANAWAKE WAOPENDWA NA WANAUME.


WENYE MSIMAMO.
Wanawake wanaopendwa, ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
WANAOJUA MAPENZI.
Wanawake wanaojua mambo ya faragha chumbani kule wanapendwa sana, sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu kitandani, mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.
MARAFIKI.
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya wanawake inayowavutia zaidi wanaume.
Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakua marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao, sio wakorofi, waungwana na wapenda amani.
WAWAZI.
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi, sio wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonyesha wanawake wa aina hii wamekua muhimu sana hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA.
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na wale naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.
WASIO NA PRESHA.
Wanawake wasio na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.
MARIDADI.
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba, wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni waelewa wa mazingira, sio washamba wanapendeza kwa muonekano.
WANAORIDHIKA.
Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekua yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.
WA MMOJA.
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waowachagua mwanzo wanahitajika sana. "nilie nae ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine" kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/aina-za-wanawake-waopendwa-na-wanaume.html

No comments:

Post a Comment