Uko na mwanaume, mmekaa kwenye mahusiano kwa miezi sita, kiola siku anakuja tu kwako na ukitaka kwenda kwake anakuzungusha zungusha, mara anakuambia anaishi nawadogo zake, mara sijui kuna hiki na kile. Lakini kuna kipindi kimoja tu alikupeleka, kufika ukakuta nguo za kike.
Akakuambia za X wake aliacha, mara za dada yake sijui alikuja, baada ya hapo hakukupeleka tena. Dada yangu huyo nu mume wa mtu na siku ambayo alikupeleka basi mke wake alisafiri. Narudia huyo ni mume wa mtu kabisa tena si wale wa kuishi na mwanamke, hapana ni wale ambao wana ndoa kama si ya kanisani ni ya msikitini.
Sijui kama umenielewa, narudia kama mwanaume alishakupeleka kwake mara moja, au anakupeleka kwa kipindi flani ila siku nyingine ukitakakwenda mara anakuambia sijui nani yupo, mara hivi mara vile huyo ni mume wa mtu tena zile ndoa ngumu. Wakati aliokupeleka mke wake alisafiri, kama huamini nenda bila taarifa utakuja kuniambia ila jua ndiyo utakanwa au unaweza kupigwa mpaka ushangae!
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/unaishije-na-mwanaume-wa-namana-hii.html
No comments:
Post a Comment