Yaani kila kitu ulichonacho umelipia, na unapotaka kununua kitu kipya unataka kiwe original na utataka na risiti. Hata ukinunua gari kwa mtu utahakikisha haijarudiwa kupigwa rangi, sio mbovu, utahakikisha hautapeleliwi, utataka Card original na File la uagizwaji ili kujihakikishia. Simu umenunua original, yaani karibu kila kitu ulichonacho umelipia.
LAKINI CHA AJABU SASA, MAMA WA WATOTO WAKO UMEMCHUKUA KIMAGENDO. HUJALIPA HATA KISHIKA UCHUMBA, WENGINE HATA BARUA YA POSA HUJAPELEKA. NA NDIO YEYE MWENYE MAANA KULIKO HATA GARI LAKO KWANI AMEKUZALIA WARITHI WAKO WATAKAOENDELEZA JINA LAKO.
LAKINI CHA AJABU SASA, MAMA WA WATOTO WAKO UMEMCHUKUA KIMAGENDO. HUJALIPA HATA KISHIKA UCHUMBA, WENGINE HATA BARUA YA POSA HUJAPELEKA. NA NDIO YEYE MWENYE MAANA KULIKO HATA GARI LAKO KWANI AMEKUZALIA WARITHI WAKO WATAKAOENDELEZA JINA LAKO.
ILA KILA SIKU UNAPIGA CHENGA KUHALALISHA UHUSIANO WENU HATA KWA KUTOA MAHARI WALAU NUSU.
KWA NINI MSIBARIKI NDOA MKAISHI KWA AMANI KIROHO NA KISHERIA? SIO LAZIMA KUFANYA HARUSI YA MAMILIONI YA HELA AMBAZO HAMNA. NENDA KALIPE MAHALI, NJOO NA SURUALI YAKO NA SHATI, MIMI NITAWABARIKIA NDOA MKAISHI KWA AMANI. MKE WAKO WALA HATAKI MAKUBWA ANATAKA TU MBARIKI MKAE KIHALALI ILI HATA KESHO MUNGU AKIKUCHUKUA AWE NA UHALALI WA KUTETEA MALI ZA WATOTO WAKO. VINGINEVYO UKIONDOKA GHAFLA NDIO ATAFURUMUSHWA HUMO NDANI NA WATOTO WAKO WATAISHI KAMA OMBA OMBA. NDUGU ZAKO WANAMUHESHIMU KWA KUWA WEWE UPO HAI. UKIFA HAKUNA RANGI HATAONA.
HIVYO, KUBARIKI NDOA SIO SWALA LA MAPOKEO NI ULINZI PIA KISHERIA KWA MWENZI WAKO MAANA VYETI VYA NDOA SIO VYA KANISA, NI VYA SEREKALI CHINI YA WIZARA YA SHERIA. NA NI HESHIMA KWA WAZAZI PANDE ZOTE MBILI.
SIJUI UNANIELEWA!?
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/wanaume-tuzungumze.html
No comments:
Post a Comment