Thursday, January 30, 2020

MAPENZI BILA UBUNIFU NA UTUNDU HAYANOGI, SOMA HII ITAKUSAIDIA UNOGESHE PENZI LAKO


Kwa asilimia kubwa mapenzi yanabebwa na utundu na ubunifu ulionao.
Ni ngumu kuteka hisia za mtu mazima kama unakosa ubunifu kwenye baadhi ya vitu na moments muhimu kwenye mahusiano.
Hebu wait kidogo, imagine umefiwa na mtu muhimu sana kwenye maisha yako.
Then mpenzi wako anakuja na kujaribu kuonyesha kiasi gani anakujali, hivyo anaamua kuchukua hatua ya kukubembeleza.
Anakusogerea karibu, na kukupapasa mgongoni huku akikuambia "Babe nyamaza, usilie. Naumia unavyolia, Be happy please".
Like seriously? Uwe happy? Wakati umefiwa? It's true ameonyesha kukujali, lakini amekosa ubunifu, maana kauli yake inaweza kukufanya umuangalie usoni na kumzaba hata kibao na kuona kama anakuletea uchuro.
Then imagine, unapitia the same situation na mpenzi wako anakuja na kukuonyesha kiasi gani anakujali na ameguswa na msiba.
Anakusogerea karibu na kukukombatia kwa nguvu.
Anakilaza kichwa chako kifuani mwake, huku akipapasa nywele zako na kukuambia kwa upole "Pole sana mpenzi wangu, najua unaumia sana. Lia babe, lia, usijizuie kulia babe, toa maumivu yote yaliyomo moyoni kisha ujitahidi kuwa strong.
Yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na hatuwezi pingana nae.
Usijutie mpenzi wangu, jitahidi uwe jasiri uweze kuvuka wakati huu mgumu unaopitia".
Anakutuliza kifuani mwake huku akiendelea kukutuliza taratibu mpaka pale unaponyamaza.
Kubwa ni kwamba, Kisaikolojia kumkombatia mtu kwa nguvu na kumuacha atulie kifuani mwako kwa dakika kadhaa, husaidia kumfanya mtu ajisikie vizuri na kumuondoa stress, depression, sadness, anxiety and pain.
Pia, usimzuie mtu kulia, muache alie akiwa kifuani mwako huku unamtuliza taratibu.
Kilio husaidia kuondoa huzuni na maumivu yaliyopo ndani ya kifua cha mtu.
Je unadhani ni mtu yupi hapo atakayebaki kwenye kumbukumbu zako wakati wote? Bila shaka ni huyu wa pili, sababu ameonyesha kukujali, na kuguswa na hali unayopitia, plus ni mbunifu.
Tusiishie hapo tu...!!!
Ladies, imagine dating a guy ambaye umezunguka nae mchana jua kali, then anakuuliza "una njaa?", kwa aibu unamjibu "Hapana", then anakuamini na kupotezea.
Kisha mfananishe na guy ambaye umezunguka nae then anakuangalia usoni na kukuambia kwa upole, "Pole sana honey, najua umechoka sana.
Twende kwanza ukale, then tumalizie mizunguko".
Kwa aibu nawe unamjibu "No sijisikii njaa". Then anakushika mkono na kukwambia "Afya yako muhimu sana. Twende ukale hivyo hivyo hata kama hujisikii njaa".
Mmefika restaurant, unakula vijiko viwili, nakujifanya umeshiba.
Anakutazama usoni, na kuupeleka mkono wake shavuni mwako.
Anakupapasa shavuni huku anakuambia "Unajua we mzuri sana, halafu unataka kujikondesha". Anachukua kijiko na kutaka kukulisha.
Unaringa kidogo, anakulazimisha kimahaba akulishe japo vijiko kadhaa. Mwisho unajikuta kakulisha mpaka sahani imeisha, kitumbo kimetuna ndii ndindi.
Yupi kati ya hao wawili utamkumbuka? Lazima itakuwa ni huyu wapili.
Why? Sababu alijua mwanamke anaweza sema NO huku moyoni akimaanisha YES.
Pia alijua mwanamke ni kama mtoto, anapenda kudekezwa, kubembelezwa.
Ndomana alionyesha utundu na mahaba kuhakikisha unakula na kuenjoy.
Imagine upo na mpenzi ambaye mnachat message 2 tu tayari story zimeisha, "Mambo"> "Poa", "Nimekumiss">"Na me pia", "Bye, nitakucheck", "okay".
Then imagine unachat na mtu ambaye story haziishi, mnachekeshana, mnataniana, mnaelimishana, mnashauriana, na kubwa zaidi mnachokozana kwa chat za mahaba.
Yani mpaka unaona kuandika ujumbe kazi, unaamua kumpigia simu ili umsikie vizuri anavyokusifia, na kukutamkia maneno yanayokutia hamu na kukuhamisha kihisia.
Yupi hapa utamuona ana umuhimu??? Bila shaka ni huyu wa pili.
Sababu ameteka hisia zako, akili yako, furaha yako, na kubwa zaidi anakufanya ujione wa thamani kwa maneno yake matamu na muda mwingi anaotenga kwaajili ya kuwasiliana na wewe.
Nimejaribu kuchukua mifano midogo sana.
Infact, upendo unanoga pale unapokuwa na mpenzi mwenye kujali na ni mbunifu, na mjuzi wa mambo.
Hebu Anza sasa, amka mapema na umjulie hali mpenzi wako pamoja na kumwambia kiasi gani unampenda.
Na hata kama sio kweli, mwambie ulimuota, tena mhadithie ndoto nzuri ya mahaba kati yako na yeye.
Kisha muage kwa mabusu na maneno matamu huku ukimsisitiza ale vizuri tena kwa wakati.
Itamfanya aanze siku kwa tabasamu.
Mpenzi wako anajua upo busy, lakini kutenga japo dakika kadhaa za kumchekesha kidogo, kuchat nae, kuhakikisha kama amekula vizuri, anaendeleaje kiafya.
Itakuwa poa sana, na itamfanya ajihisi unampenda, unamjali, na kumthamini.
Sometimes unaonyesha vurugu kidogo, unampigia simu na kumwambia kuwa ulimiss sauti yake.
Then unamvuruga hisia zake kwa kumtamkia maneno yatakayo mtia hamu ya kusex na wewe.
Itamfanya siku nzima akae akikuwaza.
Kama ndo mkeo, atatamani uwahi kurudi, kama Ndo mumeo, atatamani amalize kazi fasta aje home. Na kama bado ni wa chumba tu, basi huongeza hamu ya kutaka kukutana mara kwa mara.
Acha niishie hapa, mengine mtaongeza wenyewe huko huko mahusiano/ndoa zenu.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/mapenzi-bila-ubunifu-na-utundu-hayanogi.html

No comments:

Post a Comment