Mara nyingi ni wanawake wanakua na hii tabia ingawa hata baadhi ya wanaume wanakua nazo, ni aina ya kisirani ambacho siriasi kama unakunywa pombe unaweza kuamua tu kuhamia baaa ukirudi nyumbani unazima kabisa ili usikisikie. Kuna watu hasa wanawake wananuka kutokupendwa, ndiyo sijakosea wananuka kutokupendwa.
Ukiwa na mtu wa namna hii basi kila kitu kidogo, kila kosa utakalofanya hata kama ni lakibinadamu basi wanahisi huwapenzi; (1) Kakutumie meseji ndefu kama stori za Iddi Makengo umeshindwa kujibu huna cha kuandika maana huna maneno kichwani ukisema Thenx basi ni shida, atakua hanipendi, atakua kuna wengine anachata nao. (2) Umesahau siku yake ya kuzaliwa kwakua hata yako mwenyewe hukumbuki, eti kwakua wewe alikusapraizi wewe umesahau basi analalamika eti humpendi kwakua umesahau! (3) Ulimuambia utampigia baadaye basi umesahau imekua shida humpendi, analalamika yaani ananuna mpaka basi. (4) Anataka muongozane mpaka kwenye msiba wewe si mtu wa hivyo basi anaanza ni kwakua hunipendi? (5) Ndoa ishak0maa kabisa hakuna jipya tena, umesahau kumpigia simu kutwa nzima kwasababu ulikua bize unatukanwa na bosi wako basi akinuna ni kulalamika humpendi. (6) Uko bize zako whatsapp kwenye magroup unajadili ubora wa Ronaldo anatuma meseji, sijui hi, umekula, uko poa, hujajibu basi ni shida utakua uanchart na Malaya humpendi.
Shia ya mtu kama huyu ni kuwa unatakiwa uwe kama malaika, kwamaana ukifanya kosa lolote yeye anakimbilia humpendi, ananuna. Kila ukirudi nyumbani badala ya kuwaza nitakutana na mke wangu nitoe stress basi unaanza kuwaza hivi leo nimekosea nini maana yule mtu atakua amenuna.
Wengine sasa unafika nyumbani, kanuna hakuambii kilichomnunisha, anataka utabiri kuwa ni simu hukupokea, meseji hukujibu, au umesahau mchicha aliokutuma, au nini, yaani anakuchaganya hata na aina ya mnuno wake. Unarudi nyumbani mtu haongei hujui umekosea nini unachoona ni mashavu tu yamevimba, na usuporudi badoa tanuna kwanini hujarudi!
NIMEACHOKA KUANDIKA KAMA HUJAELEWA ENDELEA KUNUNA MASHAVU SI YAKO!
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/moja-ya-vitu-vinaboa-ni-kuwa-na.html
No comments:
Post a Comment