Siku akianza kumsifia x wake kama unavyofanya basi hata huo uanaume wako hutauona tena. Kuna baadhi ya wanaume wakioa au wakipata wapenzi wapya wana tabia ya kuwahukumu wake au wapenzi wao kwa kuangalia wapenzi wao wazamani. Utasikia mwanamke gani wewe unafanya hivi, mwenzako alikua ananifanyia hiki na hiki. Ungekua na tako kubwa kama flani, nimekuopa tu lakini akili yangu iko kwa flani, hujui kupika kama flani, nataka chakula kama flani!!! Hakuna kutu ambcho mwanamke anafanya asilinganishwe na X wake kana kwamba X au likua malaika. Mpaka wakjati mwingine unawaza mbona sasa alimuacha. Wengine wamefiwa na wake au wapenzi wao kwakua wanashindwa kuwasahau basi kila siku nikuikumbushia utafikiri hao wapenzi wapya ndiyo wamewaua! Sijui huna akili kama marehemu, marehemu angekuepo, marehemu hivi marehemu vile!
Wanaume wingu hufanya hivi wakidhanai hao wake zao labda hawana ma X wakuwazungumzia, labda wanaona kama vile wao ni Malaika na hawakosei. Nikama wanadhani kua wao ni bora kuliko ma X wa wanawake zao. Labda ukweli nikua mwanamke naye kuna nyakati anamkumbuka X wake tena sana lakini kwakua anakuheshimu na hataki ugomvi basi hunyamaza, ila nikuambie tu akuanza kumsifia X wake basi unaweza usijione mwanaume kabisa kwani anaweza sifia vitu ambavyo huna na huwezi hata kuvipata!
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/siku-akianza-kumsifia-x-wake-kama.html
No comments:
Post a Comment