Tuesday, January 28, 2020

NDOA: BUSARA ZA MAMA KWA MWANAYE


BINTI alimuuliza mama yake nifanye nini ili niwe mwenye furaha katika ndoa yangu kama ilivyo wewe na Baba yangu?
Mama yake alimjibu hakikisha unafanya mambo haya matatu.
(1) Mhifadhi mume wako, atakuwa na madhaifu mengi hayo kaa nayo na usiruhusu mtu mwingine kuyajua, tangaza mazuri yake kila akipita watu wamfurahie.
(2) Usimuombe mume wako kitu ambacho una uhakika kuwa hana uwezo wa kukupa. Ficha tamaa zako za mambo makubwa yanayozidi uwezo wake.
(3) Ongea na zika makosa yote ya awali. Akikukosea usikae na kitu rohoni, muambie kisha fukia yale yote aliyokukosea, usipande kitandani kabla ya kumsamehe na usikumbushie kosa la awali kila mara.
Ukitimiza hayo machache ndoa yako itakuwa yenye furaha daima!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/ndoa-busara-za-mama-kwa-mwanaye_28.html

No comments:

Post a Comment