1. KUWA MUWAZI kama upo tayari kuongea na ex wako mkikutana, akuulizapo swali lolote mjibu inavyotakiwa kwa majibu mafupi yasiyo ya kubabaisha yenye ukweli mtupu. Kama ni ndiyo 'ndiyo' na kama ni hapana 'hapana' itakufanya kujenga utu wako na kukupa kujiamini.
2. USIJITONGOZESHE kama umeshaachana na mpenzi wako mpya kwa sababu ya huyo mpenzi wako wa zamani usifanye mambo ya kujitongozesha kama vile kukaa naye karibu kumchekea chekea au kumtega kwa namna yeyote ile kama ikitokea bado unampenda muache yeye akuanze na umsumbue katika kumjibu kwa sababu kama mlishaachana huna hakika lile kosa halitajirudia mkirudiana.
3. KUWA NA MAWAZO CHANYA wengi wanapokuwa pamoja na wapenzi wao waliopita hufikiria negative hujiuliza anawaza nini? Ananiona mbaya? Vipi kama anakuja kunionesha mpenzi wake mpya? Haya ni maswali machache yanayowapitia wengi vichwani mwao. Lakini kama ukiwa na mawazo chanaya unaweza kujiamini na uwezo hata wa kumface huyo mpenzi wako aliyepita kwa hiyo uwapo na ex wako fikiria mawazo chanya.
4.RELAX muda mwingi watu mnapokutana na wapenzi wenu waliopita huwa mnapanic kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kutulia na kuvuta hewa nyingi ndani na kutoa nje hii hujenga kujiamini na kuondoa hofu iliyojengeka usoni mwako
5. USIONESHE KUKOSA FURAHA KATIKA PENZI LAKO LA SASA
usimpe nafasi x wako kujiona yeye ni muhimu sana katika maisha yako yaani ajione yeye alikuwa ni furaha yako ya pekee hata kama huyu wa sasa hana tofauti na yeye lakini jitahidi kujiweka sawa na kumuonehsa kuwa hakuna tatizo huyu wa zamani ili kujenga kujiamini kwako kila mnapozungumzia habari za mahusiano.source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/mambo-5-ya-kufanya-ukikutana-na-ex-wako.html
No comments:
Post a Comment