Monday, January 27, 2020

BABA LINIFUNDISHA HIVI KUHUSU WANAWAKE


"Nikufundishe nini mwanangu kuhusu wanawake? Baba yako nimezeeka ghafla nikiwa na ufahamu mdogo na mwanangu umeshakua kiasi cha kuhitaji elimu hii adhimu, nikupe neno gani?, labda hivi,
1.KUHUSU TAMAA ZAO.
-Mwanamke yeyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa Mama yako.
2. KUHUSU HULKA ZAO.
-Wanawake wote huonesha upendo wao waziwazi isipokuwa wale waliotendwa kabla.
3.KUHUSU KUACHANA.
-Mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda ni kama simba kuacha kula swala, Mwanamke kumuacha mwanaume ni rahisi kama swala kumkimbia Simba mzee.
4.KUHUSU TABIA.
-Jihadhari na maneno ya vijiweni kwamba wanawake wote wako sawa kitabia. No, lakini kumbuka hakuna Mwanamke asie Mwanamke.
5. KUHUSU MPENZI WA ZAMANI.
-Kujaribu kumsahau mwanamke uliyewahi kumpenda ni kama kumkumbuka mtu usiyemjua. Ni ngumu.
6. KUHUSU KUOA.
-Muhimu kuoa, na ni ngumu sana Kumjua mke mwema kabla ya kuoa, ni waigizaji wazuri sana. Kumbuka maneno ya Albert. " Muhimu kuoa, ukipata mke mwema utakuwa na furaha, ukipata mke mwovu utakuwa mwanafalsafa.
7. KUHUSU USALITI.
-Vizuri kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa, la usipojiandaa ama waweza kuua mtu au hata kujiua. ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote, ukijiua mwenyewe, hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulivyokuwa hai.
8.KUHUSU PESA NA MAPENZI.
-Mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi sana huko mbinguni, hapa duniani ni ngumu mno, lakini usihofu sana, kuna makubaliano bila pesa. Omba mungu.
9. KUHUSU UONGO.
-Wahenga walisema Ukweli unauma, Na mimi nakuambia "Uongo unaua"
10. KUHUSU KUWAJUA WANAWAKE.
-Ewe mwanangu, kutaka kumjua mwanamke unahitaji miaka mingi ya kuishi kuliko idadi ya nywele zao. Usihangaike na vitabu, makala, majarida, filamu, nyimbo na hotuba za wanaofundisha mandhari za wanawake. Kuna kanuni moja tu ya kupenda, " ili ubaki salama katika kupenda sharti ujipende kwanza".
...Basi mwanangu hayo ndio machache naweza kukuhusia, na wewe una nafasi ya kujifunza zaidi na kufundisha kwa ufanisi zaidi kuliko Mimi...Baba yako


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/baba-linifundisha-hivi-kuhusu-wanawake.html

No comments:

Post a Comment