Ni bora kuvumilia upweke leo hii kuliko kuharakisha kuingia kwenye NDOA au UCHUMBA na mtu asiye sahihi.
Ni ukweli usiofichika ya kwamba leo hii wengi wapo kwenye mahusiano na watu wasiowapenda sababu walikurupuka ili wakaondoe msongo wa mawazo pamoja na upweke.
Mwisho wa siku wamejikuta wameangukia pabaya zaidi na wanajutia maamuzi yao. Kumbuka ni vyema ukitoka kwenye mahusiano yaliyokuumiza upate muda wa kujitathmini ili ujue wapi ulikosea na urekebishe makosa.
Ukiingia kwenye mahusiano sababu ya kuondoa upweke na msongo wa mawazo, basi usishangae ukajiongezea maumivu, majuto, huzuni pamoja na vidonda moyoni.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/ni-bora-kuvumilia-upweke-leo-hii-kuliko.html
No comments:
Post a Comment