Monday, January 27, 2020

SIJAKUIBIA MKE WAKO NILIMUOKOTA JALALANI MWA MOYO WAKO ULIKOMTUPA NA KUMTELEKEZA KIMAPENZI.


Unakumbuka kipindi kile ulipokuwa unashinda siku nzima bila hata kumjulia hali? OTEA NI LINI HUKUMJALI!
Nilikuwa namkumbuka kila saa kujua kama yupo sawa na anaendelea vizuri.
Unakumbuka kipindi kile unamdharau na kumpuuza? Aliniambia kuhusu hilo nilijitolea kumpa muda wangu alipokuwa anahitaji kampani,nilimpa sikio langu kumsikiliza, nilimpa bega langu alipohitaji kulia na kifua changu kumfariji.
Pale ulipohisi atakufuatilia na mambo yako sisi tulikuwa bize kufurahia kampani ya kila mmoja wetu, na wewe ulikuwa mtu wa mwisho katika fikra zetu. Hivi unajua kila ulivyozidi kuumiza hisia zake ndivyo ulivyozidi kumsogeza mikononi mwangu?
Ulipodhani hatolala usiku kukuwaza na kukufikiria nilihakikisha analala bila moyo uliovunjika na kupondeka kwa kumuhadithia hadithi tamu na kumuimbia nyimbo nzuri za mapenzi.
Hivi ulidhani anakosa amani na furaha kulialia kila saa kwa ajili yako?
Hapana nilikuwa mbunifu kwa kuhakikisha anacheka na kufurahia maisha muda wote kwa ajili yake niligeuka comedian na alikuwa ni fan wangu no1
πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“πŸ’“....
Endelea kumchukulia mkeo kama takataka sisi hatuna kinyaa tutamuokota tatamsafisha na kumpa thamani.
Wengine tuna mioyo ya kike tukipenda tunapenda kweli.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/sijakuibia-mke-wako-nilimuokota.html

No comments:

Post a Comment