Monday, January 27, 2020

Kuna wakati mapenzi yanatufanya tuonekane wajinga.

Yaani unamuona kabisa mwenza wako anacheza na akili yako kama vile mtoto mdogo anavyouchezea mdoli nawe unakubali tuu.
Kutokana na kuendekeza sana hisia anakufanyia ujinga wa kutosha na usaliti wa kila aina kisha anakugeuzia kibao kesi inakua yako na kutokana na ushakua chizi wa mapenzi basi unaomba msamaha wakati makosa kafanya yeye.
Kuna wakati ukitafakari yanayoendelea kwenye mahusiano yako inabidi ujicheke na ujionee huruma ni kwa nini unaendelea kumng'ang'ania huyo mtu.
Maisha si tunaishi leo? Ila tambua na kesho ipo pia hivyo ukiongozana na mtu asiye na huruma wala kuheshimu hisia zako basi hamtaimaliza safari na mahusiano yenu yataishia njiani.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/kuna-wakati-mapenzi-yanatufanya.html

No comments:

Post a Comment