Tuesday, January 28, 2020

OGOPA SANA MWANAUME ANAYECHAT NA WEWE MPAKA SAA 8 USIKU!

Image may contain: 1 person, outdoor
Kama kuna mwanaume ambaye mmekutana online na anaweza kuchat nawe mpaka saa nane usiku basi jua kua huyo mwanaume si wako, anaweza kuwa mume wa mtu au ana mpenzi wake ambaye anampenda na wewe ni kama dawa yake. Huyo mwanaume ni mgonjwa na nikuhakikishie, narudia najua mnadhani mnapendwa lakini nakuhakikishia kama mwanaume unachat naye online, iwe ni Facebook, Instagram au Whatsapp mpaka saa nane usiku.

Nataka nirudie tena kwakua dada zangu mkikutana na wanaume wanaojibu meseji mnachanganyikiwa na kuwaona kama wanawapenda, tena akikupigia na video call ndiyo nywele zinawasisimka nakuhakikisha kua anakupenda wewe, lakini narudia na ikiwezekana mtag hata huyo mwanaume au rafiki yako ambaye anajishaua kila siku kua anapendwa “Atakua hana mtu utunachat mpaka saa nane usiku!” Kama anachat mpaka muda huo basi jua anachat na wanawake si chini ya kumi kwa wakati mmoja.

Online Psychology ya wanaume (Saikolojia ya mitandao kwa wanaume) inaonyesha kuwa mwanaume hawezi kusubiri meseji zaidi ya sekunde tano, kwa maana hiyo unapokutumia wewe wakati unamjibu anamtumia na mwingine, na mwingine, hakuna, narudia hakuna, tena hakuna mwanaume ambaye anaweza kukaa macho mpaka saa nane usiku anachat na mwanamke mmoja, hakuna tena wale wanaokuambia napenda kuchat jua wengi wanatuma meseji moja kwa wanawake zaidi ya kumi!

Tena wengi ni waume za watu na mara nyingi wanaume hawa huishia kukuambia nitumie picha zako za uchi, halafu wewe unajifanya mjanja unakatakata vipande sijui nini na kuhisi unapendwa. Kuna wanaume wengi tu wanahudumia wanawake kama ma galfriend wao katika mitandao kumbe wameoa lakini kwakua washazoea hiyo hali hawawezi kuacha ni ugonjwa. Yes kuna wanaume wengi waliooa hulala saa tisa usiku wakichat na wanawake katika mitandao, hivyo kama jana ulilala saa nane usiku ukidhani uko na mpenzi wako basi jua mlikua mko wengi!

Najua wadada mnapenda kujibiwa meseji, mnapenda wanaume wanaochat katika mitandao, ndiyo maana mnalalamika kua mume/boyfriend wangu mimi yuko online hajibu SMS zangu, nikwakua yuko bize anachat na wanawke ambao yeye huwaona kama bidhaa.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/ogopa-sana-mwanaume-anayechat-na-wewe.html

No comments:

Post a Comment