Nyie wasichana ambao hamjaolewa nyie
🚩🚩mwanaume anayekukopa kopa na halipi fyekelea mbali....Kwanza ukikutana na mwanaume anayeomba omba mwanamke hela ni janga, AKIKOPA ALIPE na usiogope kudai kisa umeahidiwa ndoa!
🚩🚩mwanaume ambaye akijua una hela anapata kihoro na atafanya namna aichukue au akushawishi muitumie au umpe yeye fyekelea mbali....
🚩🚩mwanaume ambaye hela yake huioni au hata akikupa ni kwa maneno mengi na kuzungusha kwingi na masimango mengi lakini ya kwako anaitaka tena kwa kufosi na ushawishi wa hali ya juu fyekelea mbali.....
🚩🚩mwanaume ambaye akijua una hela mapenzi yanaongezeka simu na msg kila saa mkishatumia zikaisha ubize unaingia fyekelea mbali.....
🚩🚩mwanaume ambaye shida zake ni zako tena usipomsaidia ni ugomvi lakini wewe ukipata shida hajigusi, yeye kila siku hana fyekelea mbali.....
🚩🚩mwanaume anayekushawishi ukope halafu umpe yeye wakati na yeye anaweza kukopa kimbia, hata kama hawezi kukopa lakini anakupush ukope na hana mpango wa kusaidia kulipa fyekelea mbali.....hata kama anakuambia atasaidia kulipa USITHUBUTU.....
🚩🚩mwanaume ambaye anataka umpe hela au mfanye biashara ya pamoja na hataki uulize zimetumikaje au ukiuliza anakua mkali na kutishia kusitisha mpango wa kuoa fyekelea mbali.....
🚩🚩mwanaume anayekuambia uchangie mahari au gharama za kukuoa anazotakiwa kulipa kama ipasavyo mwanaume mkimbize na panga...... *No JOINT ACCOUNTS, JOINT BUSINESSES, JOINT SEX, JOINT SIJUI KUJENGA KABLA YA NDOA......Hataki, ASEPE!
NJAA YA KUOLEWA ISIKUFANYE UKAJIPELEKA KWA CHUMA ULETE!
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/kupenda-sio-kuwa-mjinga_28.html
No comments:
Post a Comment