Wednesday, January 29, 2020

JE UNAMVULIMILIA? UNACHOKIVUMILIA KWAKE NINI? NI TABIA ZAKE AU AHADI ZAKE?


karibu twende pamoja... πŸ‘‡πŸ‘‡ Uvumilivu ndio upendo kwa kweli,huna uvumilivu huwezi kudumu kwenye mapenzi,sababu kila kiumbe kimeumbwa na udhaifu.
Tusiegemee kuumbwa kwa mapungufu ila kuna mapungufu ya sisi wenyewe kujiamria kufanya,kujiendekeza.

Mtu sahihi mwenye upendo ukubali makosa yake na kubadilika,huyu kuvumiliwa ana afadhali atakupa afya ya mahusiano,hatokupasua kichwa.
Unamvumilia mtu maiaka 10,bado haonyeshi njia kubadilika.
Leo anaomba msamaha yanaisha,kesho kutwa yupo na lingine.

Ubinafsi yeye
Uzinzi yeye.
Roporopo yeye.
Uongo yeye.

Unavumiliwa yoote bado hakuna kitu.

NGUMU KUISHI NAO.
Kuna watu wameumbwa ni vigumu kuishi nao.
Shukrani hawana,huruma hawana,upendo hawana,wafanyiwe wao mazuri sio wao kuwafanyia wenzao.
Leo anapokuambia shida yake umtekelezee papo papo,ukishindwa ni tatizo,atamaliza maneno yoote hata ya akiba.

Chake ni chake hawezi kumjua hata aliyemsaidia jana,tena si kama hana ni msiri kupindukia,mambo yake ni yakwake ila yako anataka ayajue.
Kwa nje anajipa sifa ni bonge la mtu,yuko ladhi family iangaike pesa anayo,heshima inatengenezwa nje,,huyu mwanaume.
Mwanamke yuko ladhi ajionyeshe nje mtu mwema saaana,mtakatifu mtiifu kuumbe ni mtu hovyo hafai akiwa ndani kwake.

UNAVUMILIAJE
Mpaka itokee nini ujue huyu mtu havumiliki;unapata faida gani kungoja miaka 10 yoote.
Kuwe na uvumilivu wenye ushuhuda sio uvumilivu wa kuanza clinic ya Moyo.
Moyo una kawaida ya kubeba mazito ili mwisho wake sio mzuri,utapatwa BP utapatwa misongo na uenda akili itakapochoka utaingia kwenye matatizo makubwa.

Ukisika kwenye vyombo vya habari kaua mume,kaua mke na watoto,kakata nyeti za mume wake,kajinyonga,kanywa sumu n.k.
Ni zao la uvumilivu mkubwa,uvumilivu wa muda mrefu usio na mabadiliko.
Tuvumiliane ila tuangalie na tunaowavumilia,kama wameota sugu tusijifanye makomando wa uvumilivu.
Usione shiida kuanza 1 kuliko kundelea na mtu hana faida kwako,hana msaada kokote ni kuumizana kichwa.
Na kumbuka hakuna mwanaume atakuacha umtoke wakati ulishakua katika matumizi ya kawaida yaani humwingizi hasara yoyote kazi yake ni kukudanganya danganya na kukuvua chupi..
@maisha_halisitz


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/je-unamvulimilia-unachokivumilia-kwake.html

No comments:

Post a Comment