Saturday, February 1, 2020

KUNA WAKATI HATA SIMU YAKO UNAICHUKIA.


Sababu ni yule mtu wako,no 1 wako ajatuma chochote kwa simu yako.
Yaani unaamka asubuhi hata ''Lala unono mpenzi,,uniote,nimemiss sauti yako,,nimemiss joto lako,,hakuna chochote.
Hapo sasa simu inapokeuka toi la kuchezea watoto,haina thamani kwa muda.
Unawaza weee,je hana vocha,hana data,amechoka.
ukijaribu kuangalia alikuwepo hewani muda gani,,duuuuuh unatamani Dunia ipasuke,,Dk 5 alikuwa online,,aiseeee unaweza bamiza simu ukutani.
Aiseeee,pole sana.
Kuna kitu uwa napenda nishare na nyinyi,najua maumivu ya mapenzi ni kama upepo,yanasafiri kwa nyakati na sehemu tofauti.
Ukipita kwako jiandae umalize salama ili isikuache vibaya ukakufuru Mungu,beba kama Darasa,Elimu ya kutendwa ili litakapokaribia dalili za upepo wa penzi jifunge kwenye mti uende wenyewe ukuache salama.
Jifunze ya kwamba,penzi lenye afya ni la furaha muda mwingi,sio karaha muda mwingi,Anaekukwaza sana hana upendo,jiandae kumuacha wewe sio yeye akuache.
Umuache kwa sababu ni bora kutangulia kuacha kuliko kuachwa,ni zaidi ya pigo kuachwa.
Jifunze kitu kuwa anaekuonyesha wazi hana mpango na wewe ni bora kuliko ukae na mtu vuguvugu,yupo tu aeleweki ni wa moto au wa baridi.
Kesho atakuonjesha furaha,jioni anakupa pigo tofauti,akikupiga atakufurahisha kidogo anakupiga tena,pigo takatifu,yupo yupo tu aeleweki,hawezi kukufaa mnakuwa kama watoto kwa wanaowazunguka.
Jifunze kitu kwamba,akikupiga shavu la kulia,usikubalia ageuze na upande wa pili,hakuna utakatifu huo,akikupotezea,funga,omba usiangaike nae mpaka pale uone anajibu nini jibu la wewe kumpotezea.
Kama huna thamani kwake unampaje thamani.
Kama haoni umuhimu wako vipi kwako yeye ana umuhimu,hapana.
Anauonandoa umuhimu wako kuna mtu anampa umuhimu.
Hana time na wewe kuna mtu moto umewaka yuko busy nae.
Nakupenda sana kwako haipo kuna mtu anaimbiwa Muda woote.
Mpendwa amka sasa,,!
#AnkoNimesema


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kuna-wakati-hata-simu-yako-unaichukia.html

No comments:

Post a Comment