Monday, February 24, 2020

MWILI SI MALI YAKO

Image may contain: 1 person, standing
Hii inaashiria miili yetu ni mali ya mwingine sisi tuliazimishwa tu ili itusaidie hapa duniani

Mwili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yako tuliyepewa na Mungu? Wala ninyi mwili si mali yenu
wenyewe. 1kor 6:19

Unapopangishwa nyumba unapewa masharti, maana siyo nyumba yako, nyumba yako huwezi kupewa masharti. Hata mwili si mali yako ndiyo maana Mungu anakupa masharti juu ya mwili wako.

Usilale na mke wa mwenzio, Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke ni machukizo (ushoga). Usilale na mnyama, wala mwanamke asilale na mnyama, Lawi 18:20-23

Msinyoe denge Pembeni za vichwani(kiduku). Msichanje chale yoyote ktk miili yenu, msiandike alama miilini mwenu (tatuu), Usimnajisi binti yako (usimkekete au kumcheza) kumfanya kahaba ama shoga . Lawi 19:27-29

Mwili usiufanye kiungo cha ukahaba kuufanyisha, uasherati, uzinzi zinaa za kila namna ktk duniani hii ni mwili wa kristo sio wako naongea mwili wa duniani hapa . 1kor 6 :15-18

Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanaume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke ni machukizo kwa Bwana. Adamu na Hawa walishona majini wakafanya nguo wafiche uchi wa miili yao leo nusu uchi na kuonya maungo ya miili inatoka wapi?tena . Watumishi wanao ruhusu mambo haya sheria hiyo wanatoa wapi ya ufunuo huo? Yote aliyaruhu Yesu Kirsto yameandikwa ktk Biblia . Kumb 22:5 na 1Tim 2:9a

Au tuseme Mungu anaangalia moyo si matendo na mavazi, kama hujui ndani ya moyo Kuna fikira, hisia, nia, matendo na kuvaa mavazi yanatoka ndani ya moyo wako, kama Mungu anaangalia moyo anaangalia na hayo .

Kusikia mtasikia wala hamtaelewa, Kutazama mtatazama wala hamtaona, maana mioyo ya watu hawa imefungwa na shetani imekuwa mizito wakiogopa kuongoka ili waponywe. Mat 13:14-15
Mungu amewaacha ktk tamaa za mioyo yao waufuate uchafu wa udanganyifu hata wakavunjiana heshima ya miili yao. Rumi 1:24-27

Wewe uliyeokoka vizuri kama upo ktk mambo hayo toka huko sehemu ya hao ni ktk lile ziwa liwakalo moto. Ufu 21:8
Ukiwa rafiki wa mambo ya dunia ktk mwili wako ni kuwa adui wa Mungu. Unajifanya kuwa adui wa Mungu huku ukijua au unajua maandiko yasema bure, tunapotea kwa kukosa maarifa haya ndiyo maarifa.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwili-si-mali-yako.html

No comments:

Post a Comment