πKatika maisha ya mahusiano muepuke sana mtu anaependa kukufananisha na watu wa ajabu ajabu, Muogope sana mtu anaependa kukucompare na watu wenye sifa za kijinga.
πMkwepe sana mtu anaependa kukuita majina ya ajabu ajabu, Muogope mtu anaependa kukuona wa kawaida tuu, mtu asieona jipya kwako, mtu asieona thamani yako wala kutambua utu wako.
πHuyo mtu anakudhihirishia wazi kuwa anakudharau, mtu huyo anakuona wanin, wakazi gan, huna maana. Mtu wa aina hiyo anakuangalia ovyo ovyo tuu, Yupo kwako kwa matumizi yake binafsi lakin wew si chochote, wala si lolote kwake.
πJisogeze zaidi kwa mtu anaejua umuhimu wako, mtu anaejua thamani yako, mtu anaejua bila wew yeye sio kitu. Jiweke karibu na mtu anajali utu wako, mtu anaekuthamini.
πMpende zaidi mtu anaekuona wew ni wa tofauti katikati ya watu wengine, mtu ambaye hawezi kukufananisha na chochote chini ya anga, yan kutanisha hisia zako kwa mtu anaekuona wew ni bora kuliko bora lolote chini ya jua. Hakika mtu huyo utafika nae mbali kweny safari ya mahusiano.
πUzuri na utamu wa mahusiano ni pale unapopata mtu ambae atakuheshimu, atakayekujali, atakayekuelewa, atakayejivunia kuwa na wewe, na atakayekupenda vile jinsi ulivyo.
Ambae atakuwa muaminifu kwako, atakayejua namna ya kukufariji na yule ambaye atakuvumilia bila kukata tamaa licha ya magumu fulani unayopitia.
Ambae atakuwa muaminifu kwako, atakayejua namna ya kukufariji na yule ambaye atakuvumilia bila kukata tamaa licha ya magumu fulani unayopitia.
J4REAL
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/katika-maisha-ya-mahusiano-epuka-mambo.html
No comments:
Post a Comment