Thursday, February 27, 2020

MADHARA YA KUOMBEA WATU KWA KUTUMIA MAFUTA YA UPAKO, CHUMVI YA UPAKO, VITAMBAA, SABUNI, PIPI ZA UPAKO, KEKI ZA UPAKO, MAJI YA UPAKO, DAWA YA MBU, NYOKA NK.


Madhara kwa Waombewaji:
1. Imani ya Waombewaji inahama kutoka kwa Yesu na Kuelekea kwa vitu hivyo.
2. Vinywa vya waombewaji vinataja vitambaa, mafuta zaidi kuliko Jina la Yesu.
3. Waombewaji wanakuwa kama washirikina fulani hivi (mshirikina ni mtu anayekwenda kwa waganga wa kienyeji, hata kama yeye sio mganga) nyumba zao zimejaa vichupa vya mafuta, chumvi za upako, vitambaa vya upako, yaani hivi vitu ni Hirizi wanaweka dukani, nyumbani, kwenye Magari, Mpaka kwenye Pochi zao kuna hivyo vihirizi.
Shida ikitokea hawakumbuki Jina la Yesu, ila wanakumbuka hirizi walizopewa na Waganga (Wenye Nembo ya Wahubiri).
4. Waombewaji hawana ushuhuda wa kumtukuza Yesu. Shuhuda zao zinatukuza tu hivyo vihirizi walivyopewa. Utasikia wakisema, "Ukienda kwa Nabii fulani Utapewa Mafuta ya Upako, Chumvi, Utakanyaga mafuta nk.
HAWANA USHUHUDA WA YESU.
5. Waombewaji wanamwabudu mgawa hizo Hirizi kuliko kumwabudu Yesu.
6. Waombewaji wanalinda zaidi vihirizi walivyopewa kuliko kulinda utakatifu. Yaani kwao ni bora utakatifu upotee ila chupa ya mafuta (Hirizi) isipotee.
Madhara kwa Waombeaji:
1. Waombeaji nao hawana Imani tena na Jina la Yesu ndio maana wanatafuta njia mbadala. Wanaona Jina la Yesu halitoshi.
2. Waombeaji wanahubiri zaidi vitu hivyo (Hirizi) zaidi ya kumhubiri Yesu. Utawasikia wakisema, " Ukikanyaga mafuta lazima upone, Ukiweka hiki kitambaa dukani kwako lazima wateja wengi watakuja. YAANI YESU ANAWEKWA PEMBENI.
3. Wakiombea watu wanawaaminisha kupokea miujiza kutoka kwenye vitu hivyo (Hirizi) badala ya YESU.
4. Wanatumia muda mwingi kutafuta vitu hivyo (Hirizi) kuliko wanavyomtafuta Yesu. Watavitafuta kwa gharama yeyote ile hadi wawe navyo kwenye madhabahu zao.
5. Wanatumia akili/mbinu nyingi kutengeneza vitu hivyo viwe katika namna ya kuvutia watu.
6. Wamemfanya Yesu kuwa mdogo kuliko Hirizi zao. Wakiombea watu wenye matatizo madogo madogo hawatumii hizo Hirizi. Ila wakiombea watu wenye matatizo makubwa lazima watumie Hirizi. WANAONA YESU NI WA MATATIZO MADOGO MADOGO. Yale makubwa hadi mafuta, Chumvi viwepo.
7. Waombeaji wako kibiashara zaidi kuliko huduma.
Kama Unapenda Jina la Yesu liinuliwe zaidi kuliko hizi Hirizi, SHARE KWA WINGI HUU UJUMBE. Ila Usipunguze wala usiongeze chochote.
Pastor Tumaini


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/madhara-ya-kuombea-watu-kwa-kutumia.html

No comments:

Post a Comment