Wednesday, February 26, 2020

WANAUME UPENDO WAKO USIWE UTUMWA KATIKA MAHUSIANO:

Ninapozungumzia Utumwa namaanisha, mahusiano ambayo mmoja kati yenu yupo kwaajili ya kukukomoa na wala hana mpango na wew. Mahusiano bandia ni pale mtu anapojiegesha kwako tuu kwakua anahitaji kitu Fulani.
πŸ‘‰Unakuta mtu anatambua kbsa uwezo wako mdogo kimatunzo na hata kimuonekano lakin utakuta anakuforce ufanane na uwezo wa mtu fulan, anatambu dhair huna kipato lakin anaforce umpendezeshe. Hayo ni mahusiano bandia.
πŸ‘‰Nashuhudia baadhi ya vijana hawana kabisa uwezo wa kumiliki chochote, lakin upendo wao unakua wa utumwa pale wanapopenda, Unalazimishwa kufanya kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako kwasababu tuu unampenda mtu Fulani.
πŸ‘‰Nashuhudia kuna vijana inawalazimu kuiba au kufanya vitendo vya kihalifu ili kutimiza haja ya yule ampandaye. Wakat mwingine hukumbana na maumivu na majeraha yasiyotibika ili kumlidhisha yule anaetaka kukukomoa.
πŸ‘‰Yupo msichana ambae anaona wazi mpenz wake hana chochote, hana uwezo, bado anapambana ili amilike chake, Alichojaaliwa ni upendo tuu, lakin anautumia upendo ule kuwa utumwa, anamtumikisha boy wake kupitia udhaifu wa upendo wake.
πŸ‘‰Msichana anahitaji simu kubwa wakati anajua wazi mpenz wake hana uwezo wa kuinunua, Msichana anahitaji kuvaa hiv na vile wakati anajua kbsa mtu nilie nae hana uwezo wa kunivalisha hivi. Unahitaji kuona boy wako ana gari wakat ulipompenda hukumkuta hata na baiskeli, Unauitaji kufanana na watu wa bei ghali wakati unajua uwezo wa mpenzi wako.
πŸ‘‰Dhairi shairi kuna watu wanakuja kweny mahusiano kwaajili ya kukwaruza moyo wako, kuna watu wanakuja kwaajili ya kukupa gharama usizotarajia, Kuna wengine wamejipanga kutumia upendo wako kama udhaifu wa kukutumikisha. Usikubali kuwa mtumwa katika kupenda.
πŸ‘‰Wapo watu wanashindwa kuelewa kupenda ni moyo na sio kitu kingine chochote, Utavutiwa na macho lakin upendo Unatoka kweny mzizi au shina ambalo ni moyo. Ukiona mtu anakunyanyasa kwa kuwa unampenda achana nae kwann akupe majeraha usiyotarajia.
πŸ‘‰Upendo wako usiwe chanzo cha utumwa katika mahusiano, Huna kitu chochote lakin umejaaliwa upendo kama mwanamke hatoweza kutumia upendo huo kuishi na ww ya nn akuchoshe ni dhair shairi hakupendi wala hathamin moyo wako. Ukiona dalili hiyo chomoka haraka.
J4REAL


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/wanaume-upendo-wako-usiwe-utumwa-katika.html

No comments:

Post a Comment