πKwenye mahusiano, Ukitambua kuwa kuna kukosea na kukoseana. Basi neno msamaha na samahani lazima liwe silaha ya upendo wenu.
πKwenye mahusiano ukitambua hakuna mkamilifu kati yenu basi Huruma na Kuhurumiana iwe nguzo ya upendo wenu.
πKwenye mahusiano ukitambua kuna kupewa na kupeana basi neno Asante liwe shina la upendo wenu.
πKwenye mahusiano ukitambua kwamba kuna kupata na kukosa basi subira itumike kulinda upendo wenu.
πKwenye mahusiano ukitambua kuna kuanguka na kusimama basi busara iwe mhimili wa upendo wenu
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kwenye-mahusiano-lazima-uyafahamu-haya.html
No comments:
Post a Comment