Wednesday, February 26, 2020

Yatumieni maneno haya kama kielelezo cha kutunza uhusiano wenu.

Image may contain: 4 people, wedding
📂Kwenye mahusiano, Ukitambua kuwa kuna kukosea na kukoseana. Basi neno msamaha na samahani lazima liwe silaha ya upendo wenu.

📂Kwenye mahusiano ukitambua hakuna mkamilifu kati yenu basi Huruma na Kuhurumiana iwe nguzo ya upendo wenu.

📂Kwenye mahusiano ukitambua kuna kupewa na kupeana basi neno Asante liwe shina la upendo wenu.

📂Kwenye mahusiano ukitambua kwamba kuna kupata na kukosa basi subira itumike kulinda upendo wenu.

📂Kwenye mahusiano ukitambua kuna kuanguka na kusimama basi busara iwe mhimili wa upendo wenu.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/yatumieni-maneno-haya-kama-kielelezo.html

No comments:

Post a Comment