Wednesday, February 26, 2020

JE, UNATAMANI KUACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO NA UNASHINDWA? SOMA HAPA ILI UPATE NJIA ZA KUKUSAIDIA KUACHA.



Kuacha kutazama picha za ngono kunahitaji nidhamu,
ujasiri na imani ndani yake.
Kwani bado madhara yake huwa hayaonekani mbele ya macho ya mtumiaji.
Je, kuangalia picha za ngono kuna madhara gani?
1.MAHUSIANO:

Si tu katika mahusiano yako na mchumba wako bali hata kwa marafiki,
 familia, wanafunzi wenzako, na hata wafanyakazi wenzako.
Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha wazi kuwa watu wanaoangalia picha za ngono,
 wana msongo mkubwa wa mawazo na kujihisi wapweke kuliko wasioangalia.
2.UBONGO:

Sehemu ya ubongo inaathirika na mihemko bandia inayotengenezwa  na anayeangalia,
 na hivyo kusababisha unalemaa na kushindwa kabisa kujibu mihemko halisi.
Picha hizi zitakufanya ujitenge na jamii yako, kwani kila muda utataka uwe peke,
yako eneo unalokaa ili upate wasaa wa kuangalia vizuri kwa kujinafasi.
Maisha yanakosa shauku ikiwa ubongo utazoeshwa kujibu mihemko ya bandia
 kwa kiwango cha juu.
3.KUFURAHIA MATUKIO:

Unaweza ukajikuta kila kitu kwako kinachukiza kuangalia au kujihusisha nacho,
hata ukiangalia kitu kingine utaona bora kiishe ili uangalie picha zako.
Na hii ni hatari kubwa sana kwani utaufanya ubongo ukose taarifa za ziada na zile za ngono ndio zitatawala.
Fuata hatua zifuatazo kujiachisha na tabia hii:
1.AMUA KUACHA LEO USISEME KESHO:

Mara kwa mara watu ambao wamebobea katika uangaliaji wa picha hizi,
 wanapomaliza kuangalia hujipa ahadi kwamba kesho tu nitaacha kuangalia.
Baadaye wanajikuta kesho haifiki,
 kwani kila siku ina kesho yake.
Ukitaka kweli kuacha amua muda uliopo sasa usipange kesho ambayo hujaifikia.
2.USIKAE KARIBU NA MAZINGIRA YA PICHA HIZO:

Ukitaka kujisaidia kuondokana na tatizo hili, hakikisha una kaa mazingira
 ambayo hayajatawaliwa
na picha za ngono.
Kama unatumia kompyuta, simu au
hata iPad ambayo
ndani yake umehifadhi picha hizo zifute sasa,
na ikiwa unatumuia
DVD au CD ziharibu usikae nazo ndani,
 na hata katika
historia ya anwani ya
mitandao uliyotembelea,
 kama zipo zifute kabisa kwani ukiziona utarudi kule kule.
3.USIHESABU SIKU AMBAZO HUJAANGALIA:

Mara nyingi kama umebobea kuangalia huwa haipiti siku bila
kutupia jicho picha hizo.
Na kuna muda mwingine unabanwa na shughuli nyingi kukupelekea
kufikisha siku kadhaa hujaangalia,
sasa usikae chini kuanza
kuhesabu siku ambazo hujaangalia utajikuta unajipa kibali cha
kutaka kuziangalia haraka iwezekanavyo.
4.USIKAE MAZINGIRA YA PEKE YAKO:

Mara nyingi kama uliwahi kuangalia picha za ngono na ukajikuta uko
mazingira ya peke yako,
 ya ama unaangalia tamthilia au
kusoma kitabu chochote kitakachokuwa na habari ya masuala ya watu
kujamiana itakukumbusha kamchezo kako.
Usichague pia kuangalia
 peke yako picha ziliwekwa
 alama ya miaka 18 zitakuchochea urudi ulipotoka.
5.EPUKA MAZUNGUMZO MACHAFU NA MARAFIKI:

Mara nyingi tunapokaa na marafiki zako ambao wanapenda kuhadithia
masuala ya ngono tu watakuchochea.
Maana kuna wengine ni mafundi wa kuhadithia hizo vitu,
 kana kwamba wao ndiyo watengenezaji,
sasa unapoona wanaanzisha hizo habari kama huwezi kuwasimamisha basi ni heri ujitenge nao.
6.EPUKA HISIA CHOCHEZI ZA NDANI:

Siri kubwa katika hizi picha zinampa hisia nzuri mtazamaji,
 na kuona hakuna chenye thamani yoyote muda huo.
Kwa hiyo epuka hisia za hasira,
upweke, na huzuni kwani
zitakufanya uone eneo pekee la kwenda kujipumzisha ni kuangalia picha hizo.
7.FUTA FIKRA POTOFU:

Achana na fikra potofu za mtaani kuwa kuangalia picha za
 ngono ni kujifurahisha nafsi na hazina madhara.
Lakini kiuhalisia madhara yanayoambatana na tukio lake utayaona baadaye.
Kuna wengine watakwambia kuwa usipoangalia hizo picha utakuwa mshamba na hauendi na wakati.
8.USIJISEMESHE KUWA HUWEZI KUACHA:

Unapokuwa unaangalia hizi picha mara nyingi akili yako inajizoesha,
 na kuona ni utaratibu
wake wa kila siku.
Kwa hiyo moyoni utakuwa unajisemesha kuwa kuacha kitendo hiki
hautaweza kamwe,
kitu ambacho kitakufanya uwe dhaifu wa kujitawala.
9.ACHA KUJIKUMBUSHA PICHA ULIZOANGALIA:

Mara nyingi unapokuwa mazingira fulani ya kuwaza mambo mbali mbali,
mawazo ya picha ulizoangalia ukiyatanguliza kwanza utajifanya
uwe na shauku ya kwenda kuangalia upya.
ukiona kuna kazi unafanya kazi
 katika kompyuta au umeshika kifaa chochote chenye uwezo wa kukuonesha
picha hizo ni heri ukizime
kwa muda huo halafu fikiria kitu kingine kwa haraka.
LINAPOKUJA SUALA LA KUACHA TABIA,
 HII NI VYEMA UKAFIKIRIA ZAIDI KAMA KUNA FAIDA YOYOTE UNAYOPATA.
 NA JE KUNA SIKU UTAKAYOKAA CHINI KUJIVUNIA ULICHOPATA KWA KUANGALIA HIZI PICHA? 

CHUKUA LEO HATUA YA KUACHA ILI KUEPUKA MADHARA YATAKAYOKUJA KUTOKEA SIKU ZIJAZO.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/01/je-unatamani-kuacha-kuangalia-picha-za.html

No comments:

Post a Comment