Wednesday, February 26, 2020

Mambo yanayokupasa wewe kufahamu:


|Hukatazwi Kuomba ushauri ila sio kila unachotaka kuamua ni lazima uombe ushauri, kuna mambo mengine unatakiwa kujisimamia mwenyew kusikiliza uamuzi wa kwanza kutoka kwenye msukumo wa mawazo yako. Moja ya chanzo kikubwa kinachosababisha mtu kuomba ushauri ni woga wa maamuzi, unaweza kuwa na msukumo mzuri wa maamuzi ambapo ungeamua kujifanyia mwenyew mambo yangeenda sawa lakin kitendo cha kushirikisha watu basi mambo ndio yakaharibika kabisa maana kila mtu anakuja na ushauri wake, Sio kila kitu lazima kiendeshwe na mawazo ya watu, kuna mambo ambayo unapaswa kuruhusu mamuzi yako yatawale. Kuna vitu unahitaji kusimamia mwenyew ili viende sawa. Maamuzi ya kwanza yatoke kwako, ushauri wa watu uwe ni second selection!
|Watu waliojeruhika ni wazuri kwa kukupa tahadhari ila usiwatumie kama msingi wa kujenga msimamo wa maisha yako. Kila kitu wanachoongea kimebeba ujumbe wa woga na kujihami, ukiwaendekeza utakuwa muoga wa kudhubutu na kujitoa. Unapopanda gari moja na mtu aliyewah kujeruhika na ajali anaweza kukufanya ukashuka katikati ya safari kutokana na woga pamoja na hofu, ila ukiwa na Lena ambaye ana jihami ni vizuri maana atakuepusha na madhara yasiyo ya kimsingi. Hukatazwi kuishi na watu waliojeruhika ila ishi nao kama funzo tuu na sio mpango mkakati wa kukufikisha mwisho wa safari yako!
|Kuongea na watu ni moja ya mawasiliano. Ila yakupasa kutambua unaongea na watu wa aina gani, ni nini unaongea na kwa wakati gani. Moja ya kitu ambacho watu wanafeli ni kutumia Uhuru wa kujifunua. Hukatazwi kuongea na watu, lakin sharti utambue ni nini unaongea kuna mambo ambayo si ya kuongea kwa watu, kuna mambo hayahitaji umati, kuna mambo mengine ni ya kuongea sirini sio kila jambo ni la kupayuka. Kudhibiti kauli ni jambo la kwanza ambalo litakufanya uishi na watu wote kwa usawa, Chunga Kinywa!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mambo-yanayokupasa-wewe-kufahamu.html

No comments:

Post a Comment