Friday, February 28, 2020

KWA WANAWAKE. (USIYOYAJUA KUHUSU WANAUME)


Hata namna ya kuanza kuandika ujumbe huu ni changamoto ila ukichunguza utaona asilimia zaidi ya 90 ya waalimu wanaofundisha wanawake juu ya wanaume sio wanaume bali ni wanawake wenzao. Na kwa bahati mbaya sana wengi taarifa wanazopeana zinamapungufu makubwa. Kwani kuna Sayansi ya Mwanaume ambayo anayeielewa ni mwanaume mwenyewe au mwanaume mwenzake. Huu ni ukweli usiosemwa, maana hata wanaofahamu huwa hawapendi kuongelea hilo kwa kuwastahi au kulinda hisia za walimu. Kama vile ambavyo wafundaji wengi hawana Ndoa au Ndoa zao zinachangamoto kubwa wanazokabiliana nazo. Sasa unakuta unafundishwa namna ya kuishi kwa kumvumilia mwanaume kwa methodology za mwanaume wa kungwi ambaye ni pasua kichwa na unazitumia kwa mume wako ambaye hana shida ni changamoto sana.
NGOJA NIKUIBIE SIRI. Wanaume wengi huchukuliana na vitu kwa kuangalia upepo kwenye mahusiano. Kama ukimpa uhuru wa kuwa yeye na kuwa mkweli atafunguka na kuwa huru. Ila ukimnyima uhuru ataishi sawa sawa na kiwango cha uhuru uliompa na ata-adjust kulingana na mazingira uliyoyatengeneza. Na ndipo hapo wengi wanadhani wanawajua wanaume zao ndani nje kumbe wanajua sura au mifumo ya maisha waliyoilazimisha na wanaume zao wamekubali kuendana nayo ili kuepusha ugomvi na makelele.
Mfano: Kama nikikwambia ukweli juu ya hisia zangu kwenye Jambo fulani ukaumia na kusononeka. Kesho kwenye jambo lingine napokumbuka reaction ya jana naweza nikaficha hisia zangu ili usikwazike. Na ndio hapo wanaume wengi wanaishi maisha fake kwa miaka na wenzi wao wanafikiri ndivyo walivyo. Kwaajili yako anaweza kusema “NDIO” wakati moyoni akimaanisha “HAPANA”. Anaweza kufuatilia Tamthilia asiyoipenda ili akufurahishe au apate cha kuongea na wewe. Mwanaume akikupenda anaweza akanyoa Rasta na kuvua culture akavaa suti na Tai kwaajili yako, wakati moyoni amevaa Jeans na shati la kitenge.
Wewe jaribu kumtengenezea mazingira ya uhuru wa kujieleza na kumuonesha hauumizwi na ukweli anaokwambia, mjengee tabia ya kumpa uhuru wa kuelezea hisia zake bila kumnunia kwa kusema kweli. Mruhusu awe yeye bila kulazimisha kumbadilisha atoshee picha fikirika uliyonayo kichwani. Utaanza kuona mtu mwingine mwenye furaha kuliko ulivyowahi kufikiria.
Wengi wenu waume zenu sio kama wanapenda kampani za marafiki kuliko ninyi ila kinachowakimbiza huko ni kwa sababu washkaji wanampa uhuru wa kuwa yeye bila kumnunia. Na hata wasipomuelewa bado wanabaki marafiki na maisha yanaendelea. ASIKUDANGANYE MTU, HAKUNA MWANAUME ANAPENDA KELELE NA KUNANGWA NA MWENZI WAKE, HATA KAMA HAJAWAHI KUKWAMBIA USONI ANASEMAGA MAHALI. NA HUENDA ANAVUMILIA TU KWA SABABU FULANI.
UKIMRUHUSU MWANAUME WAKO KUWA HALISI KWAKO UTAMFURAHIA. ILA UKIWA MBINAFSI NA KUMBANIA KUACHILIA HISIA ZAKE UTAJIJENGEA UKUTA KATI YENU. NA MWANAUME NI KIUMBE PEKEE AMBAYE ANAWEZA AKAKUFUTA KWENYE MAWAZO YAKE NA KUKUTOA KWENYE MAISHA YAKE NA BADO MKALALA KITANDA KIMOJA NA MKAZAA NA WATOTO. UNAPOMUONESHA KUWA HUMTHAMINI, UNAMDHARAU, UNAHISI KUJUTA KUWA NA YEYE, ANAONA, ANAJUA NA ANAWEZA HATA ASIKUULIZE, WAKATI MOYONI ANAPANGA MIPANGO YAKE.
KUWA MAKINI SANA NA KIUMBE ANAITWA MWANAUME, KUMUELEWA NI ZAIDI YA KUSOMA PhD.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kwa-wanawake-usiyoyajua-kuhusu-wanaume.html

No comments:

Post a Comment