Monday, February 24, 2020

USITHUBUTU KUMWAMBIA MANENO HAYA MPENZI WAKO!


Image result for IKIWA MWANAMKE NDIYE ANAYETAKA NDOA NA SIO WEWE KWA HITAJI LAKO KWAKE NIAMINI
Maneno Mabaya 10 ya Kutosema Kwa Mwenza Wako
Mojawapo ya nguzo kuu kabisa ya mahusiano mazuri ni mawasiliano. Mawasiliano mazuri yanahusisha vitu viwili vikubwa, kuwa na ujumbe wa kusema na namna ya kusema ujumbe wako.
Maneno ni kitu hatari sana katika mahusiano yakitumiwa vibaya na yakitumika vizuri ni nguzo kubwa ya mahusiano mazuri na yenye furaha.
Hivyo unatakiwa kupangilia maneno yako unapoongea na mwenza wako ili kupata athari chanya. Ifahamike kuwa maneno mabaya yakisha semwa hayarudi mdomoni na madhara yake yatabaki siku zote hata kama mwenza wako atasema kuwa amesamehe au kusahau.
Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vyema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile.
Maneno 10 Mabaya Ambayo Hutakiwi Kusema Kwa Mwenza Wako:
Maneno ya Matusi
Maneno kama “mjinga” au “mpumbavu” yasitumike kwa mwenza wako hata kama yana ukweli ndani yake. Japo ujinga ni kutofahamu kitu fulani lakini neno hili linaleta majeraha kama likitoka kwa mwenza. Hasa kama linatoka wakati wa ugomvi au kutofautiana.
Useseme maneno mabaya yanayomshusha mweza wako mfano kuhusu mwonekano mbaya wa mwenza wako kama “sura mbaya”,”Mnene kama nguruwe” n.k
“Nakuchukia”
Chuki ni kitu kikubwa sana,kwa kweli huwezi kuishi na mtu ambaye unamchukia. Hutakiwi kumtamkia mwenza wako neno hili. Unaweza kuchukia tabia yake lakini si yeye mwenyewe. Njia nzuri ni kusema kuwa “Nachukia au sipendi tabia yako ya kuchelewa kurudi nyumbani” au maneno yanayofanana na hayo.
“Ameiga Tabia Zako”
Wazazi wanatabia ya kurusha lawama kwa wenza wao pale watoto wanapokuwa na tabia mbaya. Utasikia mzazi mmoja akisema kwa mtoto “Tabia za mama yako hizi” au “Tabia za baba yako” pale mtoto anapoonesha tabia mbaya. Maneno haya hayafai kutumika katika familia kwakuwa yanashambulia nafsi ya mwenza wako.
Kumfananisha Tabia Mbaya za Mwenza na Wazazi Wake
“Tabia zako kama mama yako”, au “..kama baba yako” maneno yanayomfananisha mwenza wako na wazazi au familia anakotoka yanachokoza sana na huweka vidonga kwa muda mrefu moyoni na yaepukwe.
“Acha!Nitafanya Mwenyewe”
Katika mahusiano kusaidiana ni jambo la kawaida na muhimu,maneno mabaya ya namna hii yanamvunja moyo mweza wako kutaka kufanya jambo kwako siku nyingine na linaleta utengano na kuvunjika kwa upendo.
Maneno Mabaya ya Kukatisha Tamaa
“Hutaweza” ,”Hutafanikiwa” n.k yanavunja moyo kwa mwenza wako na kurudisha nyuma maendeleo.
Ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote muende mbele kwa pamoja. Umoja ni nguvu.
“Mtoto wangu”
Itambulike kuwa hakuna mtoto wa mtu mmoja,wenza wote wawili wana haki na wajibu sawa juu ya mtoto wao. Najua mila na desturi zimetufundisha tofauti juu ya haki juu ya mtoto kwa wazazi wawili lakini ukweli ni kuwa wazazi wote wana nafasi na haki sawa kwa mtoto wao.
“Haya yote ni makosa yako”
Lawama hazijengi bali zinabomoa. Lawama zinavunja moyo kwa mwenza wako. Pale panapotokea shida au matatizo kati yenu ni vyema kuyachukua kama yenu wote na mtafute suluhisho kwa pamoja.
Kutolea Mifano Mahusiano ya Zamani
Usithubuthu kumfananisha mwenza wako na mpenzi wa zamani hata kama wazamani alikuwa bora zaidi kwa vigezo vyako. Mfano “John alikuwa ananitoa sana,lakini wewe hufanyi hivyo” au “John alikuwa anapenda sana chakula hiki”
Maneno juu ya Kuachana
Usitumia maneno yanayoashiria nia ya kuachana,yanaondoa imani juu ya masiha ya mahusiano yenu.
Mfano “Kwa mtindo huu mimi nafikiri hatutafika mbali”
Mwenza wako ataanza kujiandaa kuachana na hatajiachia kwa asilimia zote kwa mapenzi na mipango ya pamoja. Maneno haya yanajenga utengano taratibu ndani ya moyo wako na wa mwenza wako.
Mwisho
Kama nilivyosema mwanzoni,mawasiliano ni nguzo ya mahusiano mazuri kati ya weza wawili. Ni kitu ambacho kila mmoja anatakiwa kujifunza na kukitilia maanani hasa kwa kujua mahusiano ya mke na mume yana changamoto kubwa kutokana na utofauti wa kihisia na kitafakuri kati ya mke na mume.
Mwanamke na mwanaume wanaonekana kama viumbe tofauti toka sayari tofauti kutokana na namna zao tofauti za kuwasiliana na kuelewa ujumbe toka kwa mwingine.
Busara za kuchambua nini cha kusema na kipi kuacha kutasaidia sana kuboresha mahusiano na mwenza wako
Nini changamoto zako na mwenza wako katika mawasiliano? Maneno mabaya yapi ambayo yanakukera kuambiwa na mweza wako na unafikiri si vyema kuyatumika kwa weza ukiacha haya? Tafadhari shiriki kujadili kwa kuandika katika kisanduku hapa chini.
Asante na nawatakia mahusiano na mwasiliano mema.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/usithubutu-kumwambia-maneno-haya-mpenzi.html

No comments:

Post a Comment