Friday, February 28, 2020

KWANINI WADADA WAZURI HUCHELEWA KUOLEWA AU KUTOOLEWA KABISA



1. Wengi wa namna hii wanajiabudu. Yaani akili zao na ufahamu wao unaishia juu ya miili yao na maumbile yao kwa kiwang ambacho akijiona au kujiangalia kwenye kioo anaona yeye hawezi kukosa mtu wa kuwa nae. Haya ni majivuno yanaozaa SELF WORSHIP, ni kiburi. Kutokana na hili, wadada wa namna hii wamekuwa wakiiingia na kutoka kwenye mahusiano kwani bado wana akili za KUJIANGALIA.

2. Kutokana na wao kujiona ni warembo wengi sana wamekuwa na kujiamini kunakopitiliza au OVERCONFIDENCE. Hii inamaanisha mdada anajiamini kuwa kutokana na uzuri alionao mkaka hawezi kumbabisha kwa lolote kwani ana uwezo wa kupata mkaka mwingine any time

3. Wadada wa namna hii pia wamefundishwa na kuandaliwa kushindana na wanaume kwani uzuri na urembo wao unakuwa kama SELF DEFENCE, kujilinda na kujikinga. Anapojiangalia anakuwa anataka mwanaume anaefanana na urembo na uzuri wake, anajikuta anachelewa na kusubiria kwani kuna wakaka hawapo bado duniani.

4. Wadada wa namna hii hujihesabia haki kuwa wanastahili kuolewa kutokana na maumbile yao kuwa ya kuvutia. Ni kweli mdada atawavutia wanaofanana nae lakini mwisho wake huwa ni maumivu ya kudumu kwa mdada.

5. Wengi wa wadada wa aina hii ni walevi wa sifa, kule kuambiwa na watu kadhaa kuwa wao ni wazuri huwa kunawafanya waendelee kuamini kuwa anaetakiwa kumuoa sio kama Raphael, mwenyewe lazima awe handsome kama yeye alivyo n kumbe Raphael alikuwa haangalii tu shape.

6. Wadada wa namna hii wanachagua au wanatumia muda mwingi sana kuchagua wakaka wanaowataka mpaka wanamkosa kila mtu na hii huwa inauma sana na hasa akiona anaolewa asiyestahili.

7. Wadada wengi wa namna hii huwa wanadhani kuolewa ni lazima uwe mrembo na mzuri kwa kila mkaka na wengi huwa wanasahau kuwa uzuri uko ndani ya macho ya anaekuona mzuri so mwisho wa siku anamkataa mkaka akiamini kuwa yeye ana uzuri

ONYO KUOLEWA SIO FASHION
KISA WATANIONAJE HEHEHEEEEE
USISHINDANE


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kwanini-wadada-wazuri-huchelewa-kuolewa_29.html

No comments:

Post a Comment