Saturday, February 1, 2020

WENYE MIMBA WOTE NA MNAOTARAJIA KUJIFUNGUA HAYA YAJUE MAJINA YA KWENYE BIBLIA NA MAANA ZAKE


Ahasuero = Mtawala, Mfalme
Amosi = Aliyesumbuliwa, Mbeba mzigo, Mwenye nguvu.
Andrea = Mwanamume.
Augusto = Anayestahili sifa
Ayubu = Mwenye kutubu
Balaamu = Mgeni
Balaki. = Muangamizaji
Barnaba = Kijana wa faraja
Benyamini = Mwana wa furaha (yaani mwana wa mkono wa kulia)
Danieli = MUNGU ni hakimu wangu
Daudi = Anayependwa,mpendwa (beloved )
Debora = Nyuki.
Delila = Anayependa kujipendekeza.
Elizabeth. = MUNGU wa kiapo, MUNGU ni kiapo
Elisha = MUNGU ni wokovu
Eliya = YEHOVA ni MUNGU
Erasto = Anayependwa
Esta = Nyota.
Eva= Kupumua, kuishi (to breath, to live )
Ezekieli = MUNGU ni mwenye nguvu au MUNGU anatia nguvu
Farao = Nyumba kubwa
Festo = Mwenye sherehe
Filemoni = Mwenye upendo. Mkarimu
Filipo = Rafiki wa farasi. Anayependa farasi
Gabrieli = Mtu wa MUNGU
Gamalieli = Zawadi ya MUNGU. MUNGU anatoa thawabu
Gideoni = Anayepiga hadi kufa.
Habakuki = kukubali, kuambatana
Hana =Kibali,Neema (favour, grace )
Haruni = Anayeangaa,aliyepandishwa juu,aliyeinuliwa juu, mlima mrefu, ( high mountain, exalted )
Hawa = Uhai.
Henoko = Kuweka wakfu
Hezekia = MUNGU ni nguvu yangu
Hosea = Wokovu.
Ibrahimu = Baba wa wengi
Imanueli = MUNGU pamoja nasi
Isaka= atafurahi, atacheka
Isakari = Yeye anatoa ajira. Ananipa mshahara
Isaya = YAHWEH anaokoa. YAHWEH ni wokovu
Ishmaeli = MUNGU anasikia maombi
Israeli = MUNGU anapigana. Anapigana na MUNGU
Jemima = Hua ( dove )
Kalebu = Mbwa
Karmeli = Bustani (ya MUNGU)
Kornelio = Mwenye pembe
Lawi = Umoja. Nia moja
Lazaro = Eleasar = MUNGU ni msaada. MUNGU amesaidia
Lea = Aliyechoka. Mwenye nguvu. Malkia wa nyumba
Lidia (Lydia ) = (mtu anayetoka)mkoa uliopo pwani ya magharibi ya Asia ndogo
Luka = Mwanga. Kuangaza
Lutu = Shera. Pazia
Magdalene = Anayetoka Magdala
Malaki = Malaika wangu. Mpeleka ujumbe
Manase = Yeye (MUNGU) amenifanya kusahau
Martha = Malkia ( the lady, the mistress )
Mathayo = Zawadi ya YEHOVA
Melkizedeki = Mfalme wa busara, Mfalme wa Amani.
Mika, Mikaya = Nani kama YEHOVA
Mikaeli = Nani Kama Mungu?, nani wa kulingana na Mungu?
Moleki = Mfalme
Mpinga Kristo = Aendaye kinyume na Kristo,Mpinzani wa Kristo,Mwalimu wa uongo, (Antichrist )
Mtume = aliyetumwa, Mjumbe
Musa = Anayevutwa juu
Naftali = Mapambano. Vita vyangu
Naomi = Uzuri wangu. Anayenipendeza. Mzuri,kupendeza, ( pleasantness )
Nathanaeli = MUNGU ametoa
Nathani = Yeye (MUNGU) ametoa
Neema = kustahilishwa,upendeleo, kupewa pasipo kustahili,kukirimiwa
Nehemia = YEHOVA anafariji
Nikodemo = Mshindi wa taifa, (kigiriki ***nike = ushindi. demos = watu)
Nuhu = pumziko, faraja
Obadia = Mtumishi wa YEHOVA
Obedi =Mtumishi, au anayeabudu
Onesimo = Mwenye faida. Anayesababisha baraka ( beneficial )
Paulo = Mdogo
Penina = Ushanga
Penueli = Uso wa MUNGU
Petro = Jiwe. Mwamba
Pilato = Aliyejiandaa kwa mkuki
Potifa = Mkuu wa walinzi
Prisila = Priska mdogo
Priska = Mzee. Anayestahili heshima,ww kale, mkongwe
Rabi = Bwana wangu
Raboni = Bwana wangu (mkuu kuzidi Rabi)
Rahabu = Paana
Raheli = Kondoo jike
Rebeka = Mtego. Anayejipendekeza
Reubeni = Yeye (BWANA) ameona unyonge wangu. An value no kijana
Roda= ua ( Rose )
Rumi = Mji wa vilima saba
Ruthu = Urafiki
Safira = Mzuri. Anayependeza
Samsoni = Mwenye nguvu. Mwenye mwanga, jua
Samweli = Aliyesikilizwa na MUNGU.
Vashti = (Mwanamke) mzuri
Sara = Anayetawala. Malkia
Sarai = Ukoo wa kifalme
Sauli = Aliyeombwa
Sefania = YEHOVA anaficha. YEHOVA ameficha
Sefari = Anaunguza. Juu. Aliyeinuliwa
Sethi = Aliyewekwa sehemu ya pili. Kulipizwa, aliyeteuliwa
Shedraki = Amri ya Aku (jina la miungu ya Babeli)
Shetani = Adui, mpinzani, aendaye kinyume na mwingine,Mshitaki ( Adversary,Complainant ,Satan Devil )
Simeoni = Kusikiliza maombi
Simoni = Kusikiliza maombi
Sinai = Kichaka chenye miiba
Sipora = Ndege (mdogo)
Stefana = Aliyevikwa taji.
Stefano = Taji
Sulemani = Mpole
Tabitha = Swala
Tera = Swala wa mlimani
Theofilo = Rafiki ya MUNGU
Timayo = Aliyeheshimiwa. Mwenye heshima
Timotheo = Anayeheshimu MUNGU
Tiro = Mwamba
Tobia = YEHOVA ni mzuri
Tomaso = Pacha
Trofimo = Anayekuzwani
Uria =Yahweh ni mwangaza wangu
Waebrania = Wanatoka pande zingine. Wavuka mpaka. Wageni
Yekonia = Aliyewekwa na Yahweh ( established by Yahweh )
Yehoshafati = YAHWEH anahukumu
Yehu = YAHWEH ni yeye
Yese = Zawadi,karama ( gift )
Yoeli = YAHWEH ni Mungu
YOHANA = YAWE ni mwenye neema
Yoshua (kiingereza > Joshua ) = YAHWEH ni wokovu NB: jina hili limetokana na neno *hoshea > Yeshua ( Aramaic language ) pia lina maana sawa na Jina la Yesu
Yusufu = ataongeza
Zebulun = Mwana wa mfalme


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/wenye-mimba-wote-na-mnaotarajia.html

No comments:

Post a Comment