Saturday, February 29, 2020

Ni rahisi kusahau maumivu ya kidonda, Lakini ni ngumu kulifuta kovu,

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Kweli kabisa ni rahisi kusahau maumivu ya kidonda, Lakini ni ngumu kulifuta kovu, Maana yake kovu ndiyo litakukumbusha chanzo cha maumivu uliyopitia wakati unaumia😭😭
UTAMKIE MOYO WAKO;
"Moyo wangu kuwa na SUBRA kila jambo huja kusababisha kujua na kujifunza, Lakini unapojifunza tengeneza njia sahihi ya kujua madhaifu yako mwenyewe yaliyopelekea kupata MAUMIVU"
Pengine ni UDHAIFU.
Pengine ni KUPENDA KUPITILIZA.
Pengine ni UWAZI ULIOPITILIZA.
Pengine ni NAMNA ULIVYO MHESHIMU.
Maana Kuna watu wengine ukimpenda sana huhisi kero, Lakini ikiwa wewe umewajibika ipasavyo kulilinda penzi lako na huoni kama unaeleweka LET GO
Huwezi kulifufua penzi lililokufa sana sana utajivika UTUMWA na mwisho kabisa uje kujutia muda uliopoteza😭😭
Kuna mtu unapokuwa muwazi yeye anachukulia kama tatizo, Kuna mtu unapokuwa mdhaifu kwake yeye anachukulia kama fimbo kukuchapia, Kuna mwingine ukimheshimu sana anaona huna pa kwenda, Ni wapumbavu pekee ndiyo huishi na akili za kijinga kiasi hicho, LOVE IS LOVE banaa, Ukipendwa unajisikia upo DUNIANI lakini ukose wa kukupenda Mbona MARADHI YOTE SUGU YATAKUPATAπŸ˜…πŸ˜…
Usimlazimishe Mtu awe nawe na ameona muda wako kwake umekwisha Nakusihi sana usijaribu kwa sababu bin adam wana tabia mbaya ya kuficha uhalisia na ndani yao wana mambo ya siri wala huwezi kujua, Mtu asiyekupenda atajitahidi kukujengea UONGO ambao utakufanya umpende na kumbe anae AMPENDAYE KWA DHATI ukija kushituka ULIISHAMPENDA lakini ndo hivyo tena kuna ambaye YUPO MOYONI MWAKE inauma sana, Kuna mijitu lina Mume/Mke kila siku kumponda ili likupe TUMAINI kumbe linaumizwa kule ndani linataka FARAJA KWAKO baadaye wakiisha ridhiana UTAKUWA FALA TU😭😭
Jifunze kuwa na Mtu wako Mwenyewe ambaye anatokana na NAFSI maana Kuna wakati tunahadaika na Macho, Moyo nao ni mdhaifu unadanganyika mwisho kabisa NI NAFSI KUHANGAIKA.
#Elista_Kasema_ila_Sio_SheriaπŸ”¨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/ni-rahisi-kusahau-maumivu-ya-kidonda.html

No comments:

Post a Comment