Wednesday, February 26, 2020

NI JAMBO ZURI KUWAZA KUHUSU NDOA LAKINI NAKUSHAURI HEBU FIKIRIA HAYA KWANZA

Linaweza likawa jambo rahisi sana kwako kufiria kuhusu NDOA, kutamani kuingia ndani ya NDOA. Lakini inawezekana pia hujafiria vyema kuhusu NDOA.
NDOA si fashion show, kwamba kila mtu aone jinsi ulivyopendeza ukiwa umevalia suti au gauni jeupe lenye nakshi za kila aina, ndoa si movie kwamba kila mtu lazima a_act kwenye kipengele atakacho, ndoa si uzuri au ubora wa picha nadhifu na zenye kuvutia kama iliyopo hapo juu.
NDOA ni taasisi imara na madhubuti inayojegwa na makubaliano ya watu wawili walioshibana na kuapa kushikamana katika hali zozote ndani ya maisha yao, kuishi kama mke na mume.
Mungu huipa baraka na utukufu ndoa takatifu iliyojaa misingi ya UPENDO, AMANI na HURUMA, na kuifanya kuwa yenye kudumu milele na milele.
Usitamani ndoa kwa kuwataza wanandoa waliovalia vizuri mavazi yao na kuonekana nadhifu katika shereheya siku moja ya ndoa yao, ila fikiria vyema ni namna gani unatakiwa kuwa baba, mama au mwanandoa ambaye utaishi na mwenza wako kwa misingi bora katika maisha yenu.
Usilazimishe ndoa kwakuwa unataka kumuumiza mwenza wako aliye tengana nawe au usitake ndoa kwakuwa umechoka kujipikia, kujifulia au umechoka kukaa kwenu.
Usiingie kwenye ndoa kwakuwa mwenza wako ana gari, nyumba nzuri na fedha ila unapaswa kusema na moyo wako kwa kina juu ya mapenzi yako kwake na mtazamo wako kuhusu maisha yenu ya baadae jinsi yatakavyo kuwa.
Usifanye maigizo kwenye maisha ya ndoa, kaa chini fikiria kwa kina, jiulize mwenyewe kwamba huu nimuda sahihi kuwa katika maisha ya ndoa?
Mtu uliye nae anamtazamo gani juu ya maisha ya ndoa?
Mtu uliye nae anataka kuingia kwenye ndoa au unamlazimisha?
Baada ya maswali hayo fanya upembuzi yakinifu kuhusu mustakabali wa maisha yako.
Ndoa sio ngumu, ugumu wa ndoa unasababishwa na wananndoa wenyewe kutokujua vyema ni yapi mahitaji ya ndoa.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/ni-jambo-zuri-kuwaza-kuhusu-ndoa-lakini.html

No comments:

Post a Comment