Kutongoza ni sanaa ambayo baadhi ya wanawake wako nayo na wengine hawana. Je ushawahi kukutana na mwanamke ambaye anaweza kumpata mwanaume yeyote bila tatizo? Tumekuandikia mwongozo wa jinisi ya kumtongoza mwanaume bila kuonekana kama unafanya hivyo.
Kabla haujaijua sanaa hio, lazima ufahamu jinsi ambavyo wanaume wenyewe hutongoza. Kwanza ni kuwa wanaume kwa kawaida hupenda wanawake wanaovutia. Hii inatumika kwa mwanaume yeyote yule. Tabia zao ni moja. So ukitaka kuteka atenshen ya mwanaume, lazima ujue jinsi ya kuvutia.
Pili lazima ujue kuwa wanaume hawawezi kutongoza kila mwanamke. Kutongoza si kitu rahisi. Wanaume wengi huogopa kuanza mazungumzo na mwanamke. Wengi wataweza kukutongoza iwapo tu utatoa ishara ya kuwa unataka kutongozwa. Sababu kuunya wanaume kushindwa kuapproach wanawake hivi hivi ni kuogopa kukataliwa na mbaya zaidi kuwa na sifa za mwanaume zege asiyekuwa na bahati kwa wanawake.
So, utaanzaje kumtongoza mwanaume bila kuonekana kama unamtogoza ili umpatie ile ishara ya kuchangamke?
#1 Onyesha tabasamu na aibu
Wanaume hupenda mwanamke ambaye anafuraha na hisia chanya. Na zaidi hupenda wanawake wanaotabasamu na kucheka wakati wanapozungumza nao. Usiongee maneno ya kuudhi ama misengenyo ukiwa na mwanaume sababu hawapendi tabia kama hizo. Pia usisahau kutabasamu na kuonyesha aibu
#2 Msifu na umshukuru
Wanaume pia hupenda kusifiwa. Kumsifia mwanaume ni mbinu ya kwanza kuanzisha mchakato mzima wa kumtongoza. Ukiona kitu kizuri kutoka huyu mwanaume basi usisite kumsifia. Pia mshukuru kwa mambo anayokufanyia. Ukimwonyesha tabia kama hizi, utakua unaanza kumtayarisha kwa mambo ambayo anapaswa kutarijia kutoka kwako hivi karibuni.
#3 Mwangalie machoni
Siri ya kujua jinsi ya kumtongoza mwanaume vizuri ni kwa kujihusisha kwa kila kitu ambacho anapenda kufanya. Si lazima uwe umefall in love na yeye ili uweze kuuteka moyonwake. Kile unachohitaji kufanya ni kumfanya awe na furaha kila wakati anapokuwa na wewe.
So wakati ambapo utakuwa umekutana naye na mnazungumza, mwangalie machoni mwake na umpe tabasamu. Kunaweza kumfanya achanyikiwe lakini mwisho utakuwa umemfanya mnyonge hadi magotini.
#4 Jionyeshe
Mwanamke ni umbo. Hivyo lazima umbo lake lionekane. Hakikisha unamakinika vizuri kwa kioo kabla kutoka kukutana naye. Jipambe vizuri, halia nguo nzuri za kuvutia. Hapa hatumaanishi unavalia nguo za uchi, la. Tunamaanisha unavalia nguo za heshima ambazo zitapendeza mtu yeyote ambaye atakuona.
Wakati mnapoongea na huyu mwanaume hakukusha unajionyesha vizuri. Mfano cheza na macho yako. Cheza na nywele zako wakati mnaongea. Hii ni moja wapo ya njia nzuri ya kumsuka mwanaume.
#5 Usiongee kwa nguvu.
Wanaume hupenda kuona ufemini kwa mwanamke. Hivyo ukiwa unaongea na huyu mwanaume hakikisha ya kuwa unaonyea kistaarabu. Sauti yako unailegeza vile ambavyo inastahili. Pia hakikisha unaongea kwa toni iliyo ya chini.
#6 Mguse mara kwa mara
Hii ndio njia nzuri zaidi ya kuhakikisha kuwa mwanaume anaingiwa na hamu ya kutaka kuongea na wewe. Wanaume hawawezi kujizuia wakati ambapo wanaihisi miguso ya wanawake ikiilisha kwa ngozi zao.
Hivyo kwa upande wako, wakati ambapo unazungumza naye, unaweza kumgusa viganja vyake, kumshika bega ama sehemu yeyote ile ambayo haitazua taharuki.
#7 Kuwa kisichana
Hapa hatumaanishi kuwa lazima ujifanye kama mtoto wa shule ili mwanaume aanze kukutongoza bali tunamaanisha kuwa unajiachilia na kumpa majukumu mwanaume ili achukue usukani. Hapa unamwacha mwanaume anakuwa kama nguzo. Usionyeshe kuwa unajua zaidi kumliko ama una akili nyingi kumliko nk. Mbinu hii utamfanya akuone uko chini yake hivyo itakuwa rahisi kwake kukutongoza haraka.
#8 Mfanye spesho
Kama umejua umuhimu wa jinsi ya kumtongoza mwanaume, basi unajua umuhimu wa kumfanya yule unayemtongoza kujihisi speshio. Hapa huhitajiki kufanya chochote kipya, lakini lazima ukumbuke kuwa ukimfanya mwanaume kujifeel spesho, basi atavutiwa na atatamani kuwa na wewe.
Mfanye ajihisi spesho kwa kumtabasamia na kumuonyesha uso wa furaha. Msifie na uwe unatumia miguso wakati mnaongea. Hapa mwanaume huyu atataka kukutongoza kwa kuwa atakuona mwanamke tofauti kati ya wote
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwanamke-jifunze-jinsi-ya-kumtongoza_29.html
No comments:
Post a Comment