Mwanamke anapopata tatizo la kihisia, ghadhabu, hasira na mfadhaiko wowote ambao unaweza kumuondolea furaha yake huhitaji kutulizwa na mume wake. Ni lazima mume utumie nafasi hii kumfariji mwenza wako kwasababu wewe ndio mtu pekee unehitajika muda huo kuonesha ni kwa jinsi gani unajali hisia na matatizo ya mkeo.
Brother. Unapomuona mkeo katika huzuni na hasira basi jaribu kuelewa hali yake. Kama ukiingia nyumbani na akawa hajakusalimu, wewe mtolee salamu. Tendo hili halitakudhalilisha wala kukuondolea uwanaume wako. Ongea naye ukiwa katika kwa busara na upole, muuleze kinacho msibu. Epuka ukali.
Akiwa katika hali amabayo si ya kawaida si vibaya ukimsaidia kazi za nyumbani. Uwe mwangalifu usimuudhi kwa namna yoyote. Usimkebehi, kama hajisikii kuzungumza, basi mwache usimlazimishe kujibu maswali yako: “Unasumbuliwa na nini?” nk.
Kama anataka kuzungumza, msikilize na mliwaze. Jifanye unahusika zaidi na tatizo lake kuliko yeye, mruhusu akwambie malalamiko yake kwako. Halafu, kama vile baba mwema au mume mwenye huruma jaribu kumsaidia apate ufumbuzi wa tatizo lake.
Mpe moyo wa kuwa mvumilivu, kwa busara na mantiki mfanye ayaone matatizo yake kama ni madogo. Imarisha tabia yake na msaidie kuvishinda vyanzo vya hasira yake, uwe mvumilivu na mtendee kufuatana na busara yako. Kwa hakika atauona msaada wako kuwa unafaa na maisha yatarudi katika hali yake ya kawaida baada ya muda mfupi kwenu nyinyi wote.
Kinyume chake, ukimwendea isivyo sahihi, inawezekana ukazidi kumsababishia mateso na maumivu makali katika moyo wake. Pia wewe utateseka na inaweza kusababisha ugomvi mkubwa ambao utawapa usumbufu wote wawili katika mahusiano yenu.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwanaume-fanya-hivi-endapo-mwanamke.html
No comments:
Post a Comment