Wednesday, February 26, 2020

Kwa wastani kama uanishi mbali na mpenzi wako,

Kwa wastani kama uanishi mbali na mpenzi wako, kama ni siku za kawaida hakuna dharura zozote wala kitu cha maana cha kuongea naye unapaswa kuongea naye si zaidi ya mara tatu kwa siku. Ingawa mawasiliano ndiyo msingi mkuu wa mahusiano ya mbali lakini yakizidi sana huwa kero.
Kumpigia pigia simu mume wako, mke wako au mpenzi wako aliyembali, ukiwa huna kitu cha maana cha kuongea, tena kw akulalamika au kutaka akusikilize wewe tu haiwi tena mapenzi inageuka na kua kero.
Hapa kuna mambo mawili, kwanza nilazima uonyeshe kua unajiamini, hapa simaanishi kumuamini hapana kua unajiamini vya kutosha na kila wakati humuwazi yeye, una kitu kingine cha maana cha kufanya ziadi ya kumuwaza yeye, lakini pili nilazima umpe pumzi na kumruhusu akumiss.
Ongea naye asubuhi ukitaka kujua hali yake, jioni kuulizia siku yake na usiku kumtakia usiku mwema na kunyegeshana. Epuka sana kuongea mchana hasa kama yeye anafanya kazi kwani si wakati mzuri, utamkuta na stress na anaweza kukujibu vibaya na kuwa mwanzo wa kuvurugika kwa penzi lenu.
Umemtumia meseji hata hajajibu basi ushampigia, umetoka kumpigia umemtumia na mesji, yuko kaitwa na bosi umepiga, hajapokea akikupigia unaulizia mbona hukupokea, mbona hujajibu, unapiga simu mara kumi kwa siku, wewe ni kero, narudia wewe ni kero.
Ndugu yangu huo si huduma kwa wateja, atakuchoka mapema, watu wanasema sukari pamoja na utamu wake kuilamba kila saa ni kero inageuka kua sumu. Kama unatabia hii kupiga simu mara kumi kwa siku, halafu hakuna hata cha maana unachoongea basi jua unamkera mwenza wako.
Kama unatabia kupiga simu mchana muda wa kazi kwakua wewe uko ‘bored’ huna kitu cha kufanya au ushamaliza kazi zako uko free unampigia wakati yeye ndiyo kwanza bosi kamsimamia au wateja wanamsumbua jua unakera na anashindwa tu kukuambia ukweli.
Kama unataka mpigie simu muda ambao unajua kabisa katulia, hana mawazo kichwa kiko safi hapo mtaelewana. Lakini kila saa wewe tu kana kwamba wewe ndiyo Oxygen yake asiposikia sauti yako anakufa, badilika.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kwa-wastani-kama-uanishi-mbali-na.html

No comments:

Post a Comment